Loading...

WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU

Loading...
WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU
link : WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU

soma pia


WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU


*Ni yule anatuhumiwa kwa utakatishaji fedha, kumiliki majumba ya kifahari

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WIZARA wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema itahakikisha inashirikiana na nchi nyingine ili kumpata Magreth Gonzaga aliyetoroka nchini Tanzania na kutokana na tuhuma zinazomkabili za utakatishaji fedha.

Gonzaga kwa sasa anatafutwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) ambapo mbali ya tuhuma za utakatishaji fedha anatuhumiwa kujipatia mali kupitia Kampuni ya Superior Financing Solution Limited inayodaiwa kufanya biashara bila kulipa kodi ya Serikali.

Akizungumza leo Machi 27 ,2019 jijini Dar es Salaam Wizara hiyo kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Sheria za kimataifa ambazo Tanzania nayo imesaini hakuna mhalifu anayeweza kutoroka nchini na asipatikane kwani kuna ushirikiano mkubwa kwa nchi mbalimbali duniani kusaidiana kutafuta wahalifu popote alipo.

"Ipo sheria maalumu ya kimataifa ambayo inahusika katika eneo la kusaidiana kutafuta wahalifu.Nchi yoyote ambaye mhalifu atakwenda atapatikana na kurejeshwa nchini na hivyo hivyo mhalifu akiwa wa nje nyingine kwa kukimbia chini atarudishwa nchi husika kwa utaratibu uliopo kisheria,"amesema Profesa Kabudi.

Hivyo amesema  mtuhumiwa Magreth Gonzaga atapatikana na atarejeshwa nchini na kwa sasa kinachoendelea ni kufuatilia kujua amekimbilia nchini gani na baada ya hapo Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria watachukua hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria na baada ya hapo Wizara ya Mambo ya Nje itachukua jukumu la kumfuatilia.

Ameongeza kwa dunia hii yenye ushirikiano katika maeneo mbalimbali hakuna mhalifu anayeweza kukimbia nchini na asipatikane, hivyo Magreth ni vema akarudi nchini na kujisalimisha Takukuru  ili sheria ichukue mkondo wake.

Alipoulizwa kama tatizo na mtuhumiwa ni kutolipa kodi ya Serikali kwanini badala ya kuhangaika kutamfuta isizungumze naye alipe kodi na kisha kuachwa akaendelea na maisha yake, Waziri Kabudi amesema kinachotakiwa mtuhumiwa huyo kutafutwa na kurejeshwa nchini na kisha hatua nyingine za kisheria zifuatwe.

"Kuna dhana kuwa kosa la kutolipa kodi ni la kawaida kwa hapa nchini kwetu, ukweli kwa nchi za wenzetu ikiwemo Ujerumani kutolipa kodi ni kosa kubwa sana na ni bora uwe na kosa la kuua kuliko kulipa kodi.Kosa la kuua unaweza hata kusamehewa lakini la kutolipa kodi halina msamaha.Hivyo badala ya kukimbia nchi ni bora akarudi tu na sheria ichukue mkondo wake,"amesema Profesa Kabudi.

Jana Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athuman alitangaza kuwa wanamtafuta Magreth ambaye ametoroka nchini wakati akitambua anatafutwa kutokana na tuhuma kwa makosa mbalimbali likiwemo la utakatishaji fedha.

Magreth Gonzaga ambaye ni Mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam anatafutwa ili kujibu tuhuma za utakatishaji fedha haramu kinyume cha kifungu namba 12(d) na 13 (a) cha sheria ya utakatishaji fedha haramu ya mwaka 2006.

Hivyo Takukuru inamsaka mwanamke huyo kupitia tangazo ambalo wamelitoa kwa vyombo vya habari.Pia inaelezwa mbali ya makosa hayo , inaeleza wakati wa uchunguzi unaendelea mtuhumiwa alitoroka nchini.

Inadaiwa kwa nyakati tofauti mtuhumiwa huyo kwa kutumia fedha ambazo ni zao la ukwepaji kodi alinunua viwanja vilivyoko ufukweni mwa Bahari ya Hindi na nyumba tatu. Pia anamiliki viwanja vitatu vilivyopo Temeke jijini.

Takukuru inasema si mara ya kwanza mtuhumiwa huyo mali zake kutolewa uamuzi wa kutaifishwa ambapo katika kesi namba CC.92/2016 alikutwa na hatia  na mali zake yakiwamo magari manne na nyumba saba zenye thaman ya Sh.milioni 486 zote zilirejeshwa serikalini .



Hivyo makala WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU

yaani makala yote WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/waziri-kabudi-amvutia-kasi-mwanamke.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU"

Post a Comment

Loading...