Loading...
title : Waziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa
link : Waziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa
Waziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amewaagiza watalaam wa wizara ya afya kuhakikisha kunakuwa na takwimu za kitaifa kuhusu hali ya usikivu nchini ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam alipokua akizungumza katika maadhimisho ya siku ya usikivu duniani ambapo katika kuadhimisha siku hiyo Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imetoa huduma ya upimaji wa usikivu bure kuanzia Machi 02 hadi Machi 03, 2019.
Amesisitiza kuwa takwimu hizo zigawanywe kwa watu wazima na watoto wenye umri wa kwenda shule ili kuisaidia Serikali kuweka afua na kuona ni jinsi gani itawawezesha watoto hao kufanya vizuri katika masomo yao.
Amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 5 ya watu duniani ambayo ni sawa na watu milioni 466 wana ukosefu wa usikivu, miongoni mwa watu hao milioni 432 ni watu wazima na milioni 34 ni watoto. Pia, inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 zaidi ya watu milioni 900 watakuwa na tatizo la usikivu.
Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wagonjwa waliohudumiwa katika Idara ya Masikio, Pua na Koo kati ya Novemba 2018 na Januari 2019 ni 5,959, kati yao 454 sawa na asilimia 8 walikuwa na tatizo la usikivu.
Amesema azma ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaendelea kuboresha upatikanaji huduma za kibingwa nchini hivyo amewataka wananchi kutoiogopa Hospitali ya Mloganzila kwa kuwa gharama za matibabu za hospitali hiyo ni sawa na za Muhimbili-Upanga.
Waziri Ummy ametumia fursa hiyo kupongeza uongozi wa Hospitali ya Mloganzila kwa kutoa huduma bora za fya na kueleza kuwa hivi sasa malalamiko yamepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokua awali.
“Niwapongeze sana kwa kazi kubwa na nzuri ya utoaji wa huduma mnayofanya, hivi sasa malalamiko ya wananchi dhidi ya Mloganzila yamepungua, nilikua napata meseji nyingi, lakini sasa hawalalamiki tena,’’amesema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani amesema MNH imekua ikifanya jitihada mbalimbali katika eneo la usikivu ikiwemo kuanzisha huduma ya upandikizaji wa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto wenye matatizo ya usikivu ambapo tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo Juni 2017, watoto 21 tayari wamepandikizwa vifaa hivyo.
Akielezea kuhusu huduma ya upimaji wa usikivu Bw. Makani amesema mpaka jana wananchi 264 wamepatiwa huduma hiyo ambapo 64 sawa na asilimia 24 wamekutwa na tatizo la usikivu na kupatiwa rufaa.
Kauli mbiu ya siku ya usikivu duniani mwaka huu ni “Chunguza Usikivu wako”
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi waliojitokeza leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila kwa ajili ya kupima kiwango cha usikivu ikiwa ni kuadhimisha siku ya usikivu duniani ambayo hufanyika Machi 3 kila mwaka.
Pichani ni wananchi waliojitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kupima kiwango cha usikivu. Baadhi ya wananchi waliofika katika hospitali hiyo wametoka mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, Morogoro na Mwanza.
Waziri wa Afya, Mhe. Mwalimu akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika kupima kiwango cha usikivu katika hospitali hiyo kutoka kwa wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makwaia Makani akizungumza katika maadhimisho hayo kabla ya kumkaribisha Waziri wa Afya, Mhe. Mwalimu kuzungumza na wananchi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Sufiani Baruani, na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mloganzila, Dkt. Mohamed Mohamed, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili.
Viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakifuatilia maadhimisho hayo leo.
Mtaalam wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Mloganzila, Dkt. Godlove Mfuko akimpima masikio Mhe. Ummy Mwalimu leo katika hospitali hiyo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua, na Koo wa Mloganzila, Dkt. Ashfag Abdulshakoor akijibu maswali ya wananchi waliofika Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kupima kiwango cha usikivu.
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakimuaga Mhe. Mwalimu leo.
Hivyo makala Waziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa
yaani makala yote Waziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/waziri-ummy-aipongeza-mloganzila.html
0 Response to "Waziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa"
Post a Comment