Loading...

AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO

Loading...
AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO
link : AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO

soma pia


AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO

DICKSON Archibold Maro (53) amekutwa amefariki dunia ndani ya gari IT, aina ya noah yenye namba za cheses 603026045 baada ya kuugua ghafla. 

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, karibu na kituo cha mafuta cha state oil, huko Mdaula, Bwilingu Chalinze mkoani Pwani. 

Alisema gari hiyo ilikuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma mkoa wa Songwe. "Baada ya kufika kituo cha mafuta cha state oil, marehemu aliugua ghafla akiwa amepaki gari eneo hilo "alifafanua Wankyo. 

Wankyo alielezea, wahudumu wa kituo hicho walitoa taarifa kwa askari polisi ambao walifika mara moja na kukuta marehemu akiwa na hali mbaya. 

Jitihada za kumuwahisha marehemu kituo cha afya Chalinze zilifanyika lakini baada ya kufikishwa kituoni hapo aligundulika amekwishafariki.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema kwamba, marehemu Dickson alipopekuliwa alikutwa na shilingi 285, 000 pamoja ,dola 400, simu mbili aina ya itel , tecno na karibu na gia kulikutwa chupa mbili za maji na chupa ya juice zilizonywewa. 

Wankyo alisema, utaratibu unafanyika kwa kushirikiana na clearance agency wanaohusika na upatikanaji wa bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine ili liweze kuondolewa kituo cha polisi Chalinze ambapo limehifadhiwa. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya Tumbi kwa uchunguzi wa daktari na ndugu wa marehemu wamejitokeza ili baada ya uchunguzi wakabidhiwe mwili huo kwaajili ya mazishi. 


Hivyo makala AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO

yaani makala yote AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/akutwa-amefariki-ndani-ya-gari-rpc.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO"

Post a Comment

Loading...