Loading...

Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza.

Loading...
Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza.
link : Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza.

soma pia


Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza.

Na.Hawa Abdalla.
ASASI za kiraia hasa zinazohusika na masuala ya utetezi wa wanawake na watoto zinapaswa kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kisiwa cha Tumbatu hasa masuala ya udhalilishaji unaowakumba wanawake na watoto wa kisiwa hicho. 

Hayo yameletwa na Mratibu wa TAMWA Zanzibar Mariam Ame  wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa maradi wa malezi mabadala unaotekelezwa katika kisiwa hicho ambapo alisema licha ya jitihada zinazochukuliwa na Serikali pamoja na Asasi za kiraia lakini bado kumeonekana kuwepo kwa mfumo dume unaosababisha watoto kukosa haki zao za msingi na kuonekana kwa malezi ya mapamoja jambo ambalo linapelekea viashiria vya hatari ya kukumbana na masuala ya udhalilishaji. 

Miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa katika utekelezaji wa Mradi huo katika kisiwa cha Tumbatu ni kuendelea kwa maswala ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ambayo hadi sasa wakazi wa kisiwa hicho wamekuwa na muhali katika kuyaripoti matukio hayo.

Alisema kwa mujibu wa Katibu tawala wa wilaya Ndogo ya Tumbatu kuna kesi nyingi ambazo hazijaripotiwa kutokana na Tabia ya wananchi wengi kujadili na kusuluhishana wenyewe kwa wenyewe. 

Alisema Tumbatu kunahitajika kutolewa elimu juu maswala ya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo jamii hiyo kujua athari zinazotokana na vitendo vya udhalilishaji kwa watoto. 

Aidha kwa Upande wake mratibu wa malezi mbadala kutoka katika Vijiji vya kulelea watoto yatima SOS Nyezuma Simai Issa alisema Mradi huo unalengo la kuwapa malezi bora kwa watoto ambao wamepoteza mzazi mmoja pamoja na familia ambazo zinaisha katika mazingira magumu. 

Alisema Mradi huo ambao unatekeleza mambo matatu ikiwemo kuwajengea uwezo wadau kuhakikisha kwamba lengo la mradi la malezi mbadala linafanikiwa Miongoni mwa wadau hao ni asasi za kirai, masheha, pamoja na maafisa kutoka serikalini. 

Aidha alisema mradi huo pia ulitenga fungu dogo katika kuboresha huduma za malezi ikiwemo elimu, Afya, na kuwapatia jamii mtaji ili kuendesha maisha yao na kulea familia zao. 

Jumla ya familia 50 katika kisiwa cha Tumbatu zimefaidika na Mradi huo wa malezi mbaladala ikiwemo watoto wa kike 29 na wakiume 21 wakiwa chini ya walezi 31. 

Mradi huo wa malezi mbadala unateekelezwa katika nchi 3 za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Rwanda, Tanzania/ Zanzibar na unaotekelezwa katika kijiji cha SOS Zanzibar kwa kushirikiana na asasi za kirai kama vile TAMWA, MUZDALIFA, na kufadhiliwa na SOS Denmark. 


Hivyo makala Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza.

yaani makala yote Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/asasi-za-kiraia-zanazojishughulisha-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Asasi za Kiraia Zanazojishughulisha na Utetezi wa Wanawake na Watoto Kuangalia Changamoto Mbalimbali Zinazojitokeza."

Post a Comment

Loading...