Loading...

CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda

Loading...
CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda
link : CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda

soma pia


CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda


Mkurugenzi wa bank ya CRDB tawi la Iringa Kissa Samweli akizungumza na wateja wa CRDB jana wakati wa warsha ya siku moja ya wanahisa juu ya kuchangamkia kutafuta fursa za kufanya kuunga mkono jitihada za serikali juu ya sera ya Tanzania ya viwanda
Mkurugenzi wa bank ya CRDB tawi la Iringa Kissa Samweli (kushoto) akimsikiliza mteja wa CRDB mfanyabiashara George Kaundama ambae ni mmoja kati ya wateja wakongwe ambao wanamiliki hisa katika bank hiyo jana wakati wa warsha ya siku moja ya wanahisa juu ya kuchangamkia kutafuta fursa za kufanya kuunga mkono jitihada za serikali juu ya sera ya Tanzania ya viwanda


washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo hayo

…………………………

NA Francis Godwin, Iringa

Benk ya CRDB imetoa rai makundi mbali mbali kama ya wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa kuchangamkia fursa ya mikopo ili kujikita kutafuta fursa ya kuendeleza ama kuboresha viwanda vidogo vidogo na viwanda vikubwa kama utekelezaji wa sera ya taifa ya Tanzania ya viwanda .

Akitoa rai hiyo wakati wa semina ya siku moja kwa umma iliyotolewa kwa wanahisa wa CRDB tawi la Irina jana mkurugenzi wa CRDB tawi la Irina Kissa Samwel alisema kuwa bank hiyo imekuwa mbele kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya viwanda kwa kutoa mikopo kwa makundi mbali mbali kwa ajili ya kuyawezesha kuboresha shughuli zao.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa aina ya mikopo ambayo wamekuwa wakiitoa ni ile ya chini kabisa ya vikundi kuanzia kiasi cha shilingi 300,000 na kuendelea pia mikopo ya wafanyabiashara wa kati na wakubwa pamoja na mikopo binafsi .

Alisema mikopo ya uendeshaji wa biashara ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya uendeshaji biashara ya kila siku kama kununua malighafi katika uzalishaji viwandani ,kununua vipuli vinavyohitajika katika matengenezo ya mara kwa mara ya mitambo ikiwa ni pamoja na kununua vitu vinavyohitajika katika usindikaji kiwandani .

Aidha mikopo hiyo hutolewa kwa ajili ya mahitaji ya gharama za uendeshaji ya kila siku kama kulipa mishahara ,gharama za maji ,umeme ,usambazaji wa bidhaa na gharama za riba ya mikopo ,mahesabu na ukaguzi na kodi na kuwa mkopo huo hutegemea mahitaji ya biashara kwa kuzingatia mtiririko wa mahesabu .

Alisema kuwa aina ya wateja ni watu binafsi ,biashara za ubia,makampuni ,biashara muunganiko ,mashirika ya umma ,vikundi na vyama vya ushirika

Makundi mengine ni azaki ,taasisi zisizo za serikali ,serikali kuu ,wakala wa serikali na wizara kuwa lazima wakopaji wawe wanaishi aum wamesajiliwa nchini Tanzania na si vinginevyo.

Aidha alisema wakopaji wasiokubalika ni watoto chini ya miaka 18 ,wale waliotangazwa kufilisika ,wasio na akili timamu ,kampuni zilizofilisika au ziko katika mchakato wa kutangazwa kufilisika hao pia hawatahusika na mikopo hiyo .

Kwani alisema lengo la CRDB kuona wenye sifa ya kunufaika na mikopo hiyo wananufaika na kuendelea kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda kwa kuwapa mikopo wote wenye sifa stahiki katika kutekeleza sera hiyo na wao kujikwamua kiuchumi.

“Mitaji iko mingi sana CRDB sera nzuri ya serikali ipo hamna sababu ya kusumbuka pia wateja wakubwa tunawakaribisha kuna mikopo mikubwa kwao kwani hakuna sababu ya kundi lolote kulalamikia mitaji kwetu mitaji iko wazi hivyo tunawakaribisha wote ili kuunga mkono juhudi za serikali na sisi wenyewe kuwa na maisha bora “ alisema mkurugenzi huyo

Mwanahisa Georege Kaundama ambae ni mmoja kati ya wafanyabiashara mkoani Iringa alipongeza CRDB kwa kuandaa semina hiyo kwa wanahisa wake na kuwa elimu iliyotolewa imewahamasisha wengi kuona sababu ya kuboresha biashara zao zaidi kwa kupitia bank hiyo .

Alisema kuwa kwa upande wake hajutii kuwa mmoja kati ya wanahisa kwani bank hiyo hataka kama uchumi umeyumba kiasi gani wamekuwa wakitoa gawio kwa wanahisa wake na hivyo silaha pekee ni kuendelea kuwepo badala ya kukimbilia bank mpya zinazoanzishwa kwani tofauti ya CRDB na hizo mpya ni ukongwe wake na mwanga ambao wanauona mbele si mwanga hafifu ni mwanga unaong’aa.

“ Imekuwa ni tabia ya kila mwanadamu anapoona kitu kipya kimekuja ama kuna usemi usemao kipya kinyemi ni lazima aende akaguse kuona ila tofauti ya CRDB toka tulipo gusa wakati huo hadi leo wao wapo imara hawayumbi wanazidi kusonga mbele “ alisema Kaundama.

Meneja Msimamizi usalama wa bank hiyo Theophel Akoro alisema kuwa sera ya viwanda iko bayana na kuwa watanzania waliowengi bado hawajajua kuwa ushiriki wao katika shughuli mbali mbali za uzalishaji iko kwenye sera ya Taifa ya kuendelea Tanzania ya viwanda .

Hata hivyo alisema kwa kuwa wengi wameshindwa kutambua vipaumbele katika sekta hiyo ambavyo wangeweza kuchukua hatua ya kuvifanyia kazi vipaumbwele hivyo ili kunufaika na sera ya Taifa ya viwanda .

Aidha alipongeza serikali ya mkoa wa Iringa kwa kutambua fursa ya uwekezaji katika uboreshaji wa miundo mbinu ya uwanja wa ndege wa Nduli pamoja na utalii kwani maeneo hayo ni sehemu kubwa zaidi yaukuzaji wa sekta ya viwanda nchini na kuwataka wananchi kila mmoja kwa uwezo wake kutafuta fursa anayoweza kunufaika nayo kuelekea Tanzania ya viwanda kama ni mkulima kusindika na kulima kisasa kama maana kilimo biashara ili kuwa mmoja wao katika endelezaji viwanda nchini. 


Hivyo makala CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda

yaani makala yote CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/crdb-iringa-yawataka-wajasiliamali-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda"

Post a Comment

Loading...