Loading...
title : DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI
link : DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI
DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MKUU wa wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani Assumpter Mshama ,amedhamiria kuyafuta mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO's) wilayani humo ambayo ni ya mifukoni huku yakifanya shughuli kwa utapeli na ubabaishaji.
Aidha amedai atayaandikia barua ya kujieleza mashirika yale ambayo yaliitwa kwenye kikao chake lakini viongozi wake hawakuweza kutokea ambapo kati ya mashirika zaidi ya 100 yaliyofika yalikuwa 21 pekee.
Assumpter aliseyama hayo wakati wa kikao chake na viongozi wa mashirika hayo ili kubadilishana mawazo na kujua changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi wao.
Alieleza, watatoa taarifa kwa wafadhili wao kuwa mashirika hayo ni ya kitapeli na hayafanyi kazi kama wanavyojieleza wanapoomba ufadhili.
"Hawa walioshindwa kuja lazima waandike barua za kujieleza kwa nini hawakufika kwenye kikao na nadhani ndo haya tunayoyasema na wakishindwa kujieleza tutawafuta na tutapeleka taarifa kwa msajili wa mashirika haya ili ayaondoe kwenye usajili," alisisitiza Assumpter.
Hata hivyo, amewataka viongozi wa mashirika hayo kupeleka taarifa zao za utendaji kazi na wawe wanatoa taarika serikalini za kila robo mwaka na ataomba wafadhili kabla ya kutoa fedha waulize juu ya mashirika hayo kwani mengine yako kwa ajili ya maslahi binafsi .
Nae ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya mji Kibaha ,Mkami Noela Hangaya alisema ,alitoa taarifa kwa mashirika yote lakini yaliyohudhuria ni machache na hakuna sababu walizotoa kwamba hawatafika.
Mwenyekiti wa shirika la kituo cha msaada wa kisheria, Kibaha (KPC) Catherine Mlenga alifafanua ,wamekuwa wakitoa taarifa serikalini ofisi ya ustawi wa jamii na kwa viongozi wa serikali za mitaa na kata hivyo wao wanafuata taratibu zote.
Hivyo makala DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI
yaani makala yote DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/dc-mshama-adhamiria-kuzifuta-ngo-s-za.html
0 Response to "DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI"
Post a Comment