Loading...
title : DC MURO AHIMIZA UCHANGIAJI WA TAASISI ZA DINI
link : DC MURO AHIMIZA UCHANGIAJI WA TAASISI ZA DINI
DC MURO AHIMIZA UCHANGIAJI WA TAASISI ZA DINI
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro amehimiza uchangiaji wa ujenzi wa majengo ya taasisi za dini na kuacha kutegemea wahisani ambao wamekuwa na masharti magumu.
Muro ametoa rai hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuchangia ujenzi wa msikiti Mdogo wa Kati uliopo Ngarenaro unaogharimu kiasi cha zaidi ya milioni 800.
Amesema ipo Haja kwa waumini kuimarisha juhudi zao wenyewe katika uchangiaji jambo ambalo litafanikisha kukamilisha ujenzi kuliko kutegemea michango ya wahisani ambayo imekuwa haifiki kwa wakati.
Muro ambaye amekubali kuwa mwanakamati wa ujenzi wa msikiti huo, ametoa kiasi cha sh,milioni 1,huku akiahidi kutoa fulana 100 kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji na ameahidi kumsomesha hadi chuo kikuu mtoto wa miaka 7, Abdulkarim Hasan baada ya kuvutiwa na uwezo wake mkubwa katika kuielewa wa dini ya kiislam.
Awali imamu wa msikiti huo,Hasan Kileo,amesema ujenzi wa msikiti huo utasaidia kuingiza idadi kubwa ya waumini tofauti na ule wanaosalia kwa sasa na utagharimu kiasi cha sh,milioni 800 nakwamba hadi sasa wamefanikiwa kupata sh,milioni 18 ambayo imetumika katika ujenzi wa msingi.
Naye sheikh Haruna Husen pamoja na kumshukuru mgeni rasm Jeri Muro kwa kuchangia ujenzi huo wa msikiti lakini aliwataka waumini wa kiislamu kuwa mstari wa mbele kujitoa katika ujenzi wa nyumba za Mungu.
Aliwataka waumini kujivunia kila walichokijenga wao kuliko kujengewa na mtu mwingine .pamoja na harambee hiyo watoto zaidia ya 50 wamehitimu elimu ya madrasa na kutakiw kufuata mema waliofundishwa
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akiwa ameketi katikati ya watoto wa madrasa wakimsomea huku wakimsomea dua.
Wanafunzi waliomaliza madrasa wakiwa wanasikiliza kwa makini hutuba ya mkuu wa wilaya
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiwa anahutubia katika harambee ya kuchangia msikiti wa Ngarenaro uliopo jijini Arusha
picha ikionyesha wa kwanza kushoto sheikh Haruna Husen akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wa tatu ni imamu wa msikiti wa Ngarenaro ,Hasan Kileo, wakiwa wanafatilia harambee hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiwa na mtoto Abdulkarim Hassan ,ambapo mkuu wa wilaya amejitolea kumsomesha mtoto huyu
Hivyo makala DC MURO AHIMIZA UCHANGIAJI WA TAASISI ZA DINI
yaani makala yote DC MURO AHIMIZA UCHANGIAJI WA TAASISI ZA DINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MURO AHIMIZA UCHANGIAJI WA TAASISI ZA DINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/dc-muro-ahimiza-uchangiaji-wa-taasisi.html
0 Response to "DC MURO AHIMIZA UCHANGIAJI WA TAASISI ZA DINI"
Post a Comment