Loading...

Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari.

Loading...
Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari.
link : Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari.

soma pia


Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari.

Msekaji Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Hospita Zanzibar Ndg. Hassan Makame, akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbli kuhusiana na matengenezo ya paa na dari la jengo la Hospital Kuu ya Mnazi mmoja, unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi yake Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar. 
Na Ramadhani Ali - Maelezo Zanzibar. 20.04.2019
Jengo kongwe la Hospitali Kuu ya Mnazimmoja linatarajiwa kufanyiwa matengenezo ya paa na dari kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Jumatano ijayo kutokna na kuvuja kwa muda kirefu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Msemaji Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Hassan Makame alisema kuvuja kwa jengo hilo kumepelekea sehemu kubwa ya dari kuharibika na kuhitaji matengenezo makubwa.
Alisema kutokana na ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Mji Mkongwe, paa la Hospitali hiyo halitavunjwa bali litafanyiwa marekebisho sehemu za misumari inayovujisha na kuwekwa misumari mipya.
Alisema hatua hiyo ni miongoni mwa juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Wizara ya Afya kuhakikisha Hospitali hiyo inafikia lengo la kuwa Hospitali ya rufaa.
Hassan aliwata wananchi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa Hospitali kutokana na usumbufu utakaojitokeza kwa sababu wagonjwa ambao hawatakuwa na sababu kubwa ya kulazwa wataruhusiwa na upasuaji unaoweza kusubiri utasogezwa siku za mbele.
Hata hivyo Msemaji huyo aliwahakikishia wananchi kuwa upasuaji wa dharura na ambao hauwezi kusubiri utafanywa wakati wote wa  matengenezo.
Katika kudumisha hali ya usafi ndani ya wodi za wagonjwa, msemaji Hassan aliwashauri jamaa wa wagonjwa wanaolazwa kuacha tabia ya kuchukua mizigo mingi kwani huduma nyingi zinapatikana hapo hapo.
Matengenezo ya paa na dari katika Hospitali kongwe ya Mnazimmoja  yatafanywa na Kampuni ya Ujenzi ya Mamba na yatagharimu shilingi milioni 154 hadi yatakapo kamilika.


Hivyo makala Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari.

yaani makala yote Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/jengo-la-hospitali-kuu-ya-mnazi-mmoja.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Jengo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Matengenezo ya Paa na Dari."

Post a Comment

Loading...