Loading...
title : KAMPUNI YA KIMATAIFA YAZINDUA MAFUNZO YA KUUZA NA KUNUNUA FEDHA KIMTANDAO
link : KAMPUNI YA KIMATAIFA YAZINDUA MAFUNZO YA KUUZA NA KUNUNUA FEDHA KIMTANDAO
KAMPUNI YA KIMATAIFA YAZINDUA MAFUNZO YA KUUZA NA KUNUNUA FEDHA KIMTANDAO
Na Khadija Seif,Globu ya jamii
KAMPUNI ya kimataifa ya kibiashara ya kuuza na kununua fedha kwenye masoko kimtandao (CITL)imeamua kuzindua mafunzo ya mfumo mpya wa kibiashara kwa lengo la kuhakikisha inawasaidia vijana kutambua ni jinsi gani wataweza kujikwamua kiuchumi kupitia biashara hiyo.
Akizungumzia mafunzo hayo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha fedha kimtandao wa kampuni hiyo Christopher Shayo amesema mafunzo hayo yataendeshwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi ili kufikisha elimu hiyo.
Shayo amefafanua mafunzo hayo yanatarajia kuanza rasmi Aprili 17,2019 na kutarajiwa kuwa na wanafunzi wapatao 100 ambao watajisajiri mapema.
Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo Jimmy James amesema mafunzo hayo yatakavowafikia watu wa mikoani pamoja na nchi zingine kupitia kwenye tovuti za kampuni ya CITL na badae kuwafikia wanafunzi hao na kuendesha mafunzo kikamilifu .
" Fursa hii ni ya kipekee kwani tumefanya tafiti na kugundua asilimia kubwa ya watu bado hawana uelewa kuhusu biashara ya kuuza na kununua fedha kupitia mtandaoni," amesema James.
Hivyo makala KAMPUNI YA KIMATAIFA YAZINDUA MAFUNZO YA KUUZA NA KUNUNUA FEDHA KIMTANDAO
yaani makala yote KAMPUNI YA KIMATAIFA YAZINDUA MAFUNZO YA KUUZA NA KUNUNUA FEDHA KIMTANDAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA KIMATAIFA YAZINDUA MAFUNZO YA KUUZA NA KUNUNUA FEDHA KIMTANDAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/kampuni-ya-kimataifa-yazindua-mafunzo.html
0 Response to "KAMPUNI YA KIMATAIFA YAZINDUA MAFUNZO YA KUUZA NA KUNUNUA FEDHA KIMTANDAO"
Post a Comment