Loading...
title : KIMBUNGA KENNETH CHAISHIA ARDHI YA MSUMBIJI, KASI YA UPEPO YAPUNGUA
link : KIMBUNGA KENNETH CHAISHIA ARDHI YA MSUMBIJI, KASI YA UPEPO YAPUNGUA
KIMBUNGA KENNETH CHAISHIA ARDHI YA MSUMBIJI, KASI YA UPEPO YAPUNGUA
*Mtwara hali shwari, wananchi washauriwa kuzidi kufuatilia taarifa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa
Na Leandra Gabriel Blogu ya jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agness Kijazi amesema kuwa kimbunga Kenneth kipo katika ardhi ya Msumbiji na kinaenda katika maeneo ya kusini na kasi ya upepo ikiwa ni kilometa 70 kwa saa huku mzingo wake ukiwa umepungua kwa kilometa 200 na hakitaweza kufika hata kwenye mpaka wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo amesema kuwa matarajio ni kwamba mgandamizo huo ni mdogo na utaendelea kupungua nguvu huku kikisogea kuelekea kusini mwa Mashariki mwa Msumbiji ifikapo mchana wa tarehe 27 Aprili na mchana wa leo tarehe 26 mgandamizo huo mdogo ulifikia kuwa umbali wa takribani kilomita 297 kusini mwa Mtwara.
Aidha amesema kuwa mgandamizo huo mdogo hautarajiwi kutua katika ardhi ya Tanzania huku ikiwa wazi kuwa sio mbali sana na mpaka wa Tanzania.
Dkt. Kijazi amesema kuwa mifumo ya hali ya hewa katika maeneo mengi ya nchi itaendeshwa na mgandamizo huo huku vipindi vya mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali vinaweza kujitokeza kufuatia mgandamizo huo.
Matazamio ya siku zijazo kwa kimbunga hicho ambazo kwa sasa ni mgandamizo Kijazi ameeleza kuwa, utarudi baharini na kikipata joto kitakuwa kimbunga kikubwa zaidi, na wao kama Mamlaka wanafuatilia kwa ukaribu ili kuweza kuzuia kutokea kwa maafa.
Maafa yaliyojitokeza kwa sehemu kilichopiga kimbunga hicho ambao nyumba na miti vimeharibiwa ni pamoja na Moeada, Muidumbe na Ilhadoibo na Mji wa Pemba nchini Msumbiji, Kisiwa cha Komoro ambapo nyumba na miti vimeathirika huku nchini Tanzania upepo ukiongezeka kwa kilomita 60 kwa saa katika maeneo ya Mtwara.
Amesema kuwa Mamlaka ya hali ya hewa itaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo mdogo wa hewa uliopo Kaskazini-mashariki mwa Msumbiji na mienendo mingine ya hali ya hewa kwa ujumla na kutoa taarifa za mrejeo kila itakapobidi.
Amewashauri wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka hiyo na kuzingatia tahadhari pamoja na kufuata ushauri na miongozo ya wataalamu katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya uratibu wa maafa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Matamwe amewashakuru wadau mbalimbali zikiwemo kampuni za simu zilizokuwa zinatoa jumbe na taarifa kwa wananchi kuhusiana na kimbunga hicho pamoja na wananchi wa Mtwara, Ruvuma na Lindi kwa kushirikiana na kamati za maafa katika maeneo yao ambapo kama kimbunga hicho kingepiga zaidi ya wakazi milioni moja wangeathirika na ametoa rai kwa kamati za maafa kote nchini kujiimarisha na kujiandaa dhidi ya majanga yoyote yanayoweza kujitokeza.

Hivyo makala KIMBUNGA KENNETH CHAISHIA ARDHI YA MSUMBIJI, KASI YA UPEPO YAPUNGUA
yaani makala yote KIMBUNGA KENNETH CHAISHIA ARDHI YA MSUMBIJI, KASI YA UPEPO YAPUNGUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIMBUNGA KENNETH CHAISHIA ARDHI YA MSUMBIJI, KASI YA UPEPO YAPUNGUA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/kimbunga-kenneth-chaishia-ardhi-ya.html
0 Response to "KIMBUNGA KENNETH CHAISHIA ARDHI YA MSUMBIJI, KASI YA UPEPO YAPUNGUA"
Post a Comment