Loading...
title : Maulamaa Watakiwa Kuwa na Hofu ya Allah Kwa Vile Wamebeba Dhima
link : Maulamaa Watakiwa Kuwa na Hofu ya Allah Kwa Vile Wamebeba Dhima
Maulamaa Watakiwa Kuwa na Hofu ya Allah Kwa Vile Wamebeba Dhima
Na.Raya Hamad .WKS.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi amelitaka Baraza la Maulamaa nchini kuwaelimisha Waumini wa Dini ya Kiislamu kuvumiliana katika tofauti ndogo ndogo na kuzipatia ufumbuzi ili amani na utulivu iendelee kutawala nchini kwa kutatua migogoro katika misingi ya Dini ya Kiislamu.
Sheikh Kaabi ameyasema hayo katika kikao cha 3 Baraza la 5 la Maulamaa Zanzibar kwenye ukumbi wa Mkutano Mazizini ambako amewasisitiza Maulamaa kuwa na khofu ya Allah kwa vile wanabeba dhima ya wanaowaongoza
"Macho imani za ya waumini wa Dini ya Kiislamu yanawatazameni nyie hivyo msiridhike na Elimu mliyonayo na ndio maana tunaambiwa tutafute Elimu mpaka uchina ili mtakapotowa hukumu na khatwa basi ziwe zinazoendana na misingi ya Dini yetu na tuiogope kalamu ya Allah "alisitiza
Aidha amewaomba Maulamaa hao kuhakikisha Maeneo wanayoyasimamia yako salama ikiwemo kuwaelewesha Maimamu namna ya kuepuka mizozo inayojitokeza ndani ya misikiti, kuwatahadharisha wageni wanaokuja kwa ajili ya kuja kutoa daawa kufuata sheria za nchi na sio kufarakanisha waumini kutokana na madhehebu .
Hivi karibuni kumezuka tabia kwa baadhi ya kikundi kukashifu viongozi wa Dini Masheikh na Maulamaa ambako wengine wamekwisha tangukia mbele ya hali na kusema kuwa si sahihi na ni marufuku kufanya hivyo .
Baraza la Maulamaa kwa kauli moja limewaagiza walimu wa Madrasa zote nchini kutowachukuwa katika sherehe na shughuli za Maulid Watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wakati wa usiku kuanzia saa 2 jambo ambalo limeelezwa linachangia kwa kiasi kikubwa udhalilishaji na ubakaji unaofanywa na baadhi ya walimu waliokosa uadilifu na utu .
Baraza limefafanua kuwa kesi nyingi za ubakaji na udhalilishaji zilizoripotiwa na kushitakiwa ambazo zimetokana na Madrasa chanzo chake ni sherehe za usiku hivyo kwa agizo hili Watoto walio chini ya umri wa miaka 18 shughuli watazopaswa kushiriki ni zile za asubuhi mpaka saa moja usiku.
Aidha Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Soraga amewaomba Masheikh kujitahidi kuwaelimisha waumini kwa njia tofauti ikiwemo kutumia khutba msikitini Vyombo vya habari, Darsa, Baraza za mazungumzo ili jamii iendelee kushikamana na Dini na kupata ufumbuzi wa baadhi ya masuala ambayo yanajibika na kutatuka bila ya kufikishana kwenye vyombo vya sheria kwa vile Baraza lina uwezo na kisheria wa kutatua migogoro na kuchukuwa uwamuzi unaofaa .
Kikao cha Maulamaa kimehudhuriwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis, Naibu Kadhi Sheikh Hassan Othman
Ngwali, Naibu Mufti Sheikh Mahmoud Wadi pamoja na Wajumbe wengine.
Kifungu cha 15 cha sheria ya Mufti nimempa Mamlaka Waziri husika kutunga kanuni ambapo miongoni mwa kanuni ni kuwepo kwa Kanuni ya Baraza la Maulamaa ya 2002.
Hivyo makala Maulamaa Watakiwa Kuwa na Hofu ya Allah Kwa Vile Wamebeba Dhima
yaani makala yote Maulamaa Watakiwa Kuwa na Hofu ya Allah Kwa Vile Wamebeba Dhima Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Maulamaa Watakiwa Kuwa na Hofu ya Allah Kwa Vile Wamebeba Dhima mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/maulamaa-watakiwa-kuwa-na-hofu-ya-allah.html
0 Response to "Maulamaa Watakiwa Kuwa na Hofu ya Allah Kwa Vile Wamebeba Dhima"
Post a Comment