Loading...

MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI.

Loading...
MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI.
link : MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI.

soma pia


MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI.

Na Estom Sanga-DSM 

Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umekutana na Wadau wa Maendeleo kutoka mashirika ya kimataifa yanayochangia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko huo. 

Katika kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Mfuko huo jijini Dar es salaam,Wadau hao wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF wamepongeza hatua ya serikali ya kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja nchini kote . 

Wamesema utekelezaji wa Mpango huo umekuwa wa manufaa na mafanikio makubwa na hivyo kuvutia mataifa mengine kuja nchini kujifunza namna Serikali kupitia TASAF ilivyotekeleza mpango huo na kuzaa matunda katika kipindi kifupi tangu kuanza kutekelezwa. 

Aidha kikao kazi hicho kimeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini inakamilika kwa ufanisi na kufanya maandalizi thabiti ya awamu ya pili inayotarajiwa kuanza katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha. 

Akizungumza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mkazo mkubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika awamu ya pili itakuwa ni kuwashirikisha walengwa wa Mpango kushiriki katika kazi kwenye miradi itakayoibuliwa kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ili kuinua kipato chao. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia hapa nchini Bwana Mohamed Muderis amesema kwa ujumla Benki ya Dunia na Washirika wengine wa Maendeleo wameridhishwa na namna Serikali ya Tanzania kupitia TASAF ilivyoonyesha dhamira ya dhati katika kutekeleza Mpango wa kunusuru Kaya maskini kwa lengo la kuboresha hali za maisha ya wananchi ambao wamekuwa wakiishi katika hali ya umaskini . 

Menejimenti ya TASAF na wadau wa maendeleo hukutana mara moja kila mwezi kufanya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa lengo la kuhakikisha kuwa utekelezaji huo unakuwa wa manufaa kwa Walengwa .

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bw. Ladislaus Mwamanga (mbele) akiongoza kikao kazi cha menejimenti na Wadau wa Maendeleo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia nchini Bw. Mohamed Muders (aliyesimama akizungumza kwenye kikao kazi kati ya menejimenti ya TASAF na Wadau wa Maendeleo) kushoto kwake ni mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga .

Baadhi ya Wadau wa maendeleo na menejimenti ta TASAF (picha ya juu na chini ) wakiwa katika kikao kazi kilichojadili utekelezaji wa shughuli za TASAF.






Hivyo makala MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI.

yaani makala yote MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/menejimenti-ya-tasaf-yakutana-na-wadau.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI."

Post a Comment

Loading...