Loading...

MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA

Loading...
MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA
link : MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA

soma pia


MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA

Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki Dodoma Beatus Kinyaiya amewataka Vijana kuwa mstari wa mbele kwenye kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii,kiuchumi na kisiasa ili kuijenga na kuistawisha Tanzania kwa kuwa ndio kundi kubwa linalotegemewa kwa kiasi kikubwa kwenye Kusukuma ajenda mbalimbali za kimaendeleo.

Baba Askofu Kinyaiya ameyasema hayo jana wakati wa adhimisho la Ibada ya Jumapili ya Matawi katika Kanisa la Mt. Yohana Mtume Kikuyu,Dodoma ambapo pia siku hii huwa ni maalum kwa ajili ya VIJANA WAKATOLIKI ULIMWENGUNI na kwa jana ilisimamiwa na VIJANA WAKATOLIKI WAFANYAKAZI*(VIWAWA)*

“Vijana wa Kanisa muwe mfano bora,ishini katika haki,upendo na kujituma na msiwe wasaliti wa nafsi zenu.Mfanye kazi kwa bidii na kujituma kwani Taifa linawategemea.Nimefurahi juu ya uanzishwaji wa Kituo cha Vijana ambacho kitatoa pia mafunzo ya Ufundi,jukumu la kukamilika kwake namuachia kijana mwenzenu Anthony Mavunde”-Alisisitiza Baba Askofu Mkuu Kinyaiya

Akizungumza katika Ibada hiyo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ,amewahidi Vijana hao kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha ujenzi wa kituo hicho na akachangia Mifuko 100 ya saruji na fedha Tsh 1,000,000 na kuongoza harambee iliyopelekea kupatikana matofali 7000 ili ujenzi wa ukuta kuzunguka kituo uanze mara moja na pia kutoa ahadi ya kuwapatia vifaranga 500 kwa ajili ya mradi wa Kuku wa Mayai ili waweze kujiendesha kiuchumi.

“Baba Askofu Mkuu,mimi katika maisha yangu muda mrefu nilikuwa mtumishi wa Altareni kanisani na nimekuwa sehemu ya VIWAWA,namuomba Mungu atusaidie yote tuliyopanga leo yatimie ili kituo hichi kiwasaidie Vijana wengi hasa katika kutatua changamoto ya ukosefu wa Ajira”-Alisema Mavunde






Hivyo makala MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA

yaani makala yote MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/mhashamu-baba-askofu-mkuu-beatus.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA"

Post a Comment

Loading...