Loading...

MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE

Loading...
MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE
link : MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE

soma pia


MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE

Na Dkt. Muhammed Seif Khatib
Saa kumi na mbili magharibi. Tarehe kama ya leo. Unyama ulifanyika. Unyama ulifanyika wa kuutorosha uhai. Kutorosha uhai mbichi wa mkombozi wa Waafrika wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.Yalikuwa mauaji ya kikatili ya kummiminia darzeni nzima ya risasi ya mtu aliyekuwa hana silaha ya kujilinda.Mwuwaji ni mwaajiriwa wa Serekali.Mwuwaji aliyekula kiapo cha utii cha uaskari cha kuilinda Taifa na viongozi wake. 

Hiki kilikuwa kisasi cha kurithi kwa muuwaji huyu kutoka kwa baba yake?Kama ni hivyo sababu ya mauaji ya kikatili ni ileile ya baba wa muuwaji huyu?Mwaka 1946 serekali ya kikoloni iliitoa nafasi ya ushiriki katika Bunge la Zanzibar kwa wawakilishi wa wananchi ya kuteuliwa kwa misingi ya kikabila ya Waarabu watatu,Wahindi wawili,Mzungu mmoja na Mshirazi(Mwaafrika) mmoja.

Jumuia ya African Association ya Zanzibar ikalalamikia kunyimwa kwa nafasi za kutosha za uwakilishi ya Waafrika ambao ndiyo wengi na wenye asili ya Zanzibar.Wakaloni na Sultani mwaka 1950 wakafanya mabadiliko ya uwakilishi katika Baraza la kutunga sheria ya kuteua Waarabu wanne,Waafrika wanne,Wahindi watatu na Mzungu mmoja.

Usawa huu wajumbe wanne wa Waarabu na Waafrika ukaikera sana Jumuia ya Kiarabu ya Zanzibar na kuamua kuvisusia vikao Baraza.Ikatokea mmoja ya Waarabu aitwaye Ahmed Mugheiry kutokubaliana na Waarabu wenzake waliotaka idadi ya Waafrika ipunguzwe na isiwe sawa na ya Waarabu.

Mughery akasusiwa na Waarabu wenzake.Kundi la Waarabu wakamjeruhi kwa visu.Mughery akaharakishwa hospital ya Mnazi Mmoja kwa matibabu.Wakati anapatiwa matibabu, Mwarabu Mohammed Barwani akiigiza kuwa ndugu wa mgonjwa Mughery akaingia wodini na kuchomoa kisu na kumchoma tumboni na kifuani hadi kufa kwa kosa la kutetea Waafrika.

Huyu muuwaji Mohammed Barwani ndiye aliyemzaa muuwaji wa Abeid Karume aitwaye Homoud Mohammed Barwani kwa bunduki ya kivita miaka 22 baadaye tarehe kama ya leo.Huu ukoo wa mauaji ya kikatili yumkini katika damu yao na nafsi yao wana chuki dhidi ya Waafrika wa Zanzibar.Kwa nini baba na mtoto waue viongozi wanaotetea masilahi ya Waafrika wanyonge, kundi lilokosa fursa na haki za msingi katika ardhi ya nchi yao?

Kosa la Abeid Karume kwa muuwaji Homoud ni kupigania haki ya Waafrika?Waafrika wa Zanzibar kabla kufanikwa kwa Mapinduzi ya Januari mwaka 1964 yaliyoongozwa na Abeid Karume walilazimishwa na utawala wa Kiarabu wa Kisultani wawe watu duni.Ni wao waljofanywa watumwa na kugeuzwa bidhaa ya kuuzwa sokoni.

Mwaka 1859 katika soko la watumwa Zanzibar bei ya mtumwa mtoto ni sh.25 na mtu mzima sh.45. Na kwamba mwaka 1840 kiasi ya watumwa hao millioni moja na laki sita waliuzwa nje ya Zanzibar.Waafrika hawa Zanzibar ndiyo walioimarisha mashambaya minazi na Karafuu iliyokuwa inamilikiwa na mabepari wa Kiarabu.

Majengo makubwa ya kihistoria leo katika Mji Mkongwe na Kasir nyingi za Sultan tofauti zimejengwa kwa nguvu za Waafrika wa Zanzibar.Kwa miaka nenda miaka rudi wachumaji wa karafuu na wakwezi wa minazi katika mashamba walikuwa Waafrika.Marobota kwa marobota ya mazao ya karafuu na mbata kwa miaka kadha ikibwebwa katika migongo iiliyoota masuguru ya wachukuzi na makuli Waafrika.

Mji Mkongwe ulikuwa unakaliwa na Masultani, Waarabu, ,Wazungu na Wahindi matajiri.Hata hivyo, wapishi wao,madobi wao,mayaya wao na matopasi wao walikuwa Waafrika kutoka mitaa ya ng'ambo.Masultani na Waarabu matajiri walistarehesha na matamanio ya miili yao kwa wanawake wa Kiafrika waliowabatiza kwa jina la ‘ masuria’ bila kuwaoa.

Ingawa Waafrika ndio nchi yao Zanzibar walibaguliwa katika kila kitu.Walinyimwa kumiliki ardhi na mashamba.Elimu walikoseshwa huku Waarabu na Wahindi wakijenga na kuendesha skuli zao za makabila.Huduma za elimu za msingi zilikuwa za kulipia ambapo Waafrika walikosa fedha za kulipia.

Wale waliokuwa wanaishi mjini katika mitaa duni isiyokuwa na miundombinu wala fursa walitakiwa walipiye kodi ya viwanja kwa vibanda vya kuishi.Waafrika wengi walikufa kwa kukosa huduma za kiafya na lishe.Kwa matokeo hayo Waafrika wa Zanzibar kuajiriwa katika za serekali na kubaki kuwa matarishi na wafagiaji katika maofisi ya srekali kwa miaka nenda
miaka rudi.

Ni Karume na chama cha Afro – Shirazi waliokuja kuleta Mapinduzi ya kuondoa dhuluma hii na kurejesha utu na heshima ya Mwafrika.Kumbe bado wapo watu wanaotaka Mwaafrika awe mtwana,mjakazi na suria katika Zanzibar.Mohammed Barwani na mwanawe Homoud Mohammed Barwani hawataki mabadiliko hayo.Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuuwawa Karume.Wauwaji hatuwasahau na hatuwasamehe.


Hivyo makala MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE

yaani makala yote MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/miaka-47-ya-kifo-cha-hayati-abeid-aman.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE"

Post a Comment

Loading...