Loading...
title :
link :
Na.Othman Khamis OMPR.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuwajali wananchi wake Unguja na Pemba kwa kuanzisha na kuendeleza miradi mbali mbali itakayozalisha ajira kwa wingi kwa wananchi hasa Vijana wanaomaliza masomo yao ili waweze kujiajiri na kuondokana na umaskini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Shaaban Seif Mohamed alieleza hayo wakati alipokuwa katika ziara maalum huko Mkoa wa kusini Unguja ya kukagua miradi iliobuniwa na wananchi kupitia mradi wa TASAF awamu ya tatu ili kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi hao kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.
Katibu Shaaban alisema, serikali kuu haina uwezo wa kuwapatia ajira wananchi wake wote ndio maana ikaamua kuweka utaratibu mzuri wa kuanzisha miradi na kuwapa fursa wananchi hao kubuni mipango watakayoifanya ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Nd. Shaaban alisema, serikali imekuja na mradi wa TASAF kupitia awamu tofauti ikiwa na lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo umaskini, kipato duni, ukosefu wa ajira hivyo amewaomba wananchi hao kuzithamini jitihada hizo za serikali ili waweze kufikia lengo lililokusudiwa.
“Niseme tu serikali yenu ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Mhe. Dk Ali Mohamed Shein inawajali na kuwathamini wananchi wake ndio maana imekuwa ikibuni njia nyingi zitakazowawezesha nyinyi kujiimarisha kiuchumi” Alieleza Katibu Shaaban.
Pamoja na mambo mengine Katibu Shaabani akiwa katika ziara hiyo aliwataka wananchi hao waliojikusanya katika vikundi kuachana na tabia ya muhali kwa wale watu wasiowahurumia kwa kuiachia mifugo kuharibu mazao yao kwani kutofanya hivyo kutawasaidia kupata kipato juu ya shughuli wanazozifanya.
Ameleza kuwa kutokana na changamoto inayowakabili ya wafugaji kuachia mifugo yao ovyo hatimae kuingia katika mashamba yao ni lazima waipatie ufumbuzi kwa kushirikiana na serikali ya Shehia kwa kuanzisha sheria ndogo ndogo (By Laws) zitakazowabana wafugaji hao pindi mifugo yao itakapoharibu mazao walioyazalisha.
“Lazima muondokane na muhali kwa watu ambao wamekua na tabia ya kuwarudisheni nyuma kwa kuwaharibieni mazao yenu kwa kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana kwa kushirikiana na serikali yenu ya shehia” Alisema Katibu huyo.
Akisoma taarifa maalum ya wananchi wa shehia ya Muyuni “C” Naibu Sheha wa shehia hiyo Hassan Amour Ali amesema mradi wa TASAF awamu ya tatu umeleta tija kwa wananchi kwani yapo mafanikio makubwa ikiwemo kupatikana kwa kipato na kugaiwa kwa kila mwanakaya husika.
Naibu sheha Hassan alisema mbali na mafanikio hao yaliyopatikana lakini pia walengwa wamefanikiwa kupatiwa elimu ya kuweka akiba na kukuza uchumi ambapo jumla ya vikundi vitano katika shehia ya Muyuni “C” wamepatiwa elimu sambamba na uanzishwaji shamba za uzalishaji wa vitalu vya miembe na migomba.
“Kwa kweli Ndugu Katibu mkuu sisi wananchi wa shehia ya Muyuni “C” tumenufanika na kufanikiwa moja kwa moja na mpango huu wa kunusuru kaya Maskini Kupitia TASAF”. Alisema Naibu Sheha Hassan.
Kwa upande wake mwananchi kutoka shehia ya Muyuni “C” Bi Mwanaidi amemuomba Katibu Mkuu kuwapatia ufumbuzi wa Changamoto zinazowakabili ikiwemo kuongezewa eneo la kilimo ili waweze kuzalisha zaidi pamoja na Kuzungushiwa uzio katika eneo lao ili kuyalinda mazingira hayo kuvamiwa na wanyama kama vile Ngo’mbe na Mbuzi.
Nae mratibu kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais anaesimamia mpango wa kunusuru kaya Maskini (TASAF) Makame Ali Haji amewataka wananchi walionufaika na mpango huo kuiendeleza miradi hiyo kwa kuitumia vyema elimu na ujuzi waliyoipata kutokana na mafunzo mbali mbali waliopatiwa.
Mratibu Makame alisema kumekuwepo na tatizo kubwa kwa baadhi ya wananchi kuacha kuiendeleza miradi ilioanzishwa mara baada ya kumalizika muda wake jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za serikali katika kufikia malengo yake ya kuzinusuru kaya maskini ziweze kujitegemea.
“Pamoja na lengo la mradi kuwapatia ajira wananchi lakini kumekuwepo na changamoto ya kutoiendeleza miradi mara ya kupitwa na muda wake” Alieleza Mratibu Makame.
Ziara hiyo ya Katibu mkuu imejumuisha shehia za Kitogani, Muyuni “C” na Kizimkazi Dimbani ambapo amepata fursa ya kutembelea miradi ya Kilimo iliyobuniwa na wanakaya husika.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/na.html
0 Response to " "
Post a Comment