Loading...

Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019

Loading...
Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019
link : Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019

soma pia


Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019



Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akitembezwa na wahandisi na viongozi wa TBA kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam alipofanya ziara yake leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (kulia) akipata maelezo kwenye chumba cha kuendeshea mtambo wa kuchakata zege katika mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam alipofanya ziara yake leo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Eng. Jasper Lugemarila (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) alipofanya ziara leo kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Eng. Jasper Lugemarila (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (wa pili kulia) alipofanya ziara leo kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota. Wengine ni wahandisi wa mradi huo.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) akitoka katika moja ya majengo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam alipofanya ziara yake leo.

……………………

NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa ameagiza Wakala wa Majengo Nchini (TBA) kuhakikisha wanamaliza Mradi wa Nyumba za Kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam unamalizika kufikia mwezi Desemba mwaka huu.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Kwandikwa ametoa msisitizo huo leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kukagua maendeleo ya mradi huo.

Amesema kuanzia sasa atakuwa akiutembelea mradi huo kila mwezi ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na hatimaye mradi ukamilike Desemba kama ilivyoagizwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli alipoutembelea mradi huo hivi karibuni.

“…Kuanzia leo nitahakikisha nawatembelea hapa kama sio kila wiki basi kila mwezi, lengo langu ni kuhakikisha mradi huu mkubwa unakamilika kwa wakati na wananchi hawa wapatao 656 waliokuwa wakiishi hapa wanaingia na kuanza kuzitumia nyumba hizi,” alisema Naibu Waziri.

Aidha aliongeza kuwa wizara yake itahakikisha inafika eneo hilo kila mara kutatua changamoto zote ambazo zitakuwa zikihitaji kutatuliwa na wizara hiyo, huku akionya itakuwa ni jambo la kushangaza endapo mradi huo utasimama tena na kumlazimu Rais Dk. Magufuli arudi tena eneo hilo.

“…Sisi kama wizara tunataka endapo Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli akija tena eneo la Magomeni Kota ni kufanya uzinduzi wa nyumba zikiwa zimekamilika na si vinginevyo,” alisisitiza Naibu Waziri Kwandikwa akizungumza na viongozi na waandisi wa TBA wanaosimamia mradi huo.

Aliipongeza TBA kwa kitendo cha kuanza kutumia mitambo ya kisasa ya kufyatua matofali, kuchanganya na kubeba zege hadi gorofani jambo ambalo litaongeza kasi ya ujenzi na ufanisi katika mradi huo.

Aliwataka kuangalia namna ya kuanza haraka kufanya kazi usiku na mchana kutokana na ujio wa mitambo hiyo. Alisema wazo la kuanza kufanya kazi usiku na mchana licha ya kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi linatoa fursa kwa vijana wengi sasa kuja kufanya kazi na kujipatia kipato.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Eng. Jasper Lugemarila akizungumzia changamoto zilizokwamisha mradi huo awali, alisema ilikuwa ni kupanda kwa bei ya zege ambayo walikuwa wakinunua pamoja na bidhaa nyingine kama simenti, kokoto na nondo.

Alisema kwa sasa wamekwisha tatua changamoto hizo baadha ya kuanza kutengeneza zege wenyewe kwa kutumia mitambo ya kisasa inayoendeshwa na kompyuta.

“…Mwanzoni tulikuwa tunamimina zege kwa kununua kutoka kwa wafanyabiashara hiyo, lakini walipoona mradi huu umeanza na ni mkubwa wakatupandishia bei sana wakijua lazima twende kwao,” alisema Eng. Jasper Lugemarila


Hivyo makala Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019

yaani makala yote Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/naibu-waziri-kwandikwa-asisitiza-mradi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Naibu Waziri Kwandikwa Asisitiza Mradi wa Nyumba za Kisasa Magomeni Kota Ukamilike Desemba, 2019"

Post a Comment

Loading...