Loading...
title : POLISI ARUSHA WAJENGA NYUMBA ZAO SIKU YA MUUNGANO
link : POLISI ARUSHA WAJENGA NYUMBA ZAO SIKU YA MUUNGANO
POLISI ARUSHA WAJENGA NYUMBA ZAO SIKU YA MUUNGANO
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akishiriki kubeba matofali wakati wa ujenzi wa nyumba za askari polisi eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za Muungano.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Jonathani Shana akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kushiriki ujenzi wa nyumba Sita za Polisi eneo la Njiro mjiani Arusha jana ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Sherehe za Muungano.
Askari na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wakishiriki usaombaji wa matofauri wakati wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa askari hao eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sherehe za Muungano.
Askari Polisi wakiwa chini ya msingi kwa ajili ya kumwaga zege wakati wa ujenzi wa nyumba za askari eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Muungano.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mwenye jacket akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Jonathan Shana wakishiriki kubeba zege wakati wa ujenzi wa nyumba za polisi eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya sherehe za Muungano.
Askari na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wakishiriki usaombaji wa matofauri wakati wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa askari hao eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sherehe za Muungano.
ASKARI wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamesheherekea Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanziba kwa kushiriki ujenzi wa nyumba Sita za makazi ya askari polisi eneo la Njiro mjini Arusha.
Ujenzi huo uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana na maofisa wa polisi mkoani humo walioshiriki kubeba matofali na kumwaga zege kwenye msingi za nyumba hizo.
Akizungumza eneo la tukio RC Gambo alisema serikali ya mkoa itaendelea kuhakikisha inaondoa changamoto ya ukosefu wa makazi bora kwa askari wake hatua itakayowawezesha kufanya kazi kwa utulivu na umakini zaidi.
Naye Kamanda Shana alimshukuru Rais Dk. John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Nsiro kwa kuendelea kuboresha makazi ya askari mkoani humo.
Ujenzi wa nyumba hizo Sita unatarajiwa kuchukua familia Sita za watu takribani 5 kwa nyumba na hivyo kufanya kuwa na watu takribani 30 watakaoishi kwenye nyumba hizo.
|
Hivyo makala POLISI ARUSHA WAJENGA NYUMBA ZAO SIKU YA MUUNGANO
yaani makala yote POLISI ARUSHA WAJENGA NYUMBA ZAO SIKU YA MUUNGANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI ARUSHA WAJENGA NYUMBA ZAO SIKU YA MUUNGANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/polisi-arusha-wajenga-nyumba-zao-siku.html
0 Response to "POLISI ARUSHA WAJENGA NYUMBA ZAO SIKU YA MUUNGANO"
Post a Comment