Loading...

SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

Loading...
SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI
link : SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

soma pia


SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

WAZIRI wa  Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Januari Makamba amesema kwamba katazo la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki nchini litakuwa la kisheria na kanuni zake zitakazokuwa na adhabu kwa wale watakaokiuka.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Makamba pia amesema katika kipindi hichi cha mpito,wizara yake itaweka utaratibu wa mahali pa kuiweka,sehemu ya kuisalimisha na kuiteketeza kwa walio na mifuko hiyo katika magodauni yao kabla haijawa kosa kisheria kwa muda uliowekwa na Serikali.

Kwa kukumbusha tu,mapema wiki iliyopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa bungeni Mjini Dododma,alisema kuanzia Juni Mosi mwaka huu, itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuuza, kuingiza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote.

Hivyo Waziri Makamba wakati anazungumza na wadau wa mifuko ya plasiki, kuhusu fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mifuko mbadala ya plastiki amefafanua katazo hilo litakuwa la kisheria na sio tamko.

Ameongeza kuwa katazo hilo  ni kuanzia uzalishaji, kuuza, kuingiza, kumiliki, kuhifadhi kutumia,yote hayo ni makosa.Kanuni hizo watakazoweka zitakuwa na adhabu kwa watakaokiuka hata atakayekutwa naye na kutakuwa na faini au vifungo kwa mujibu wa sheria,kanuni zitakapokamilika zitatangazwa"alisema Makamba

Pia amesema katazo hilo halitausisha vifungashio vya plastiki kwa bidhaa kama Korosho,maziwa, na nyinginezo bali litaanza kwa mifuko ya plastiki inayotumika kubebea bidhaa.

Wakati huo huo Makamba amesema uwamuzi wa katazo hilo si wa gafla kama inavyosemwa na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki kwani inafahamika tangu Agosti mwaka 2016 kwa wadau kuandikiwa barua kujadili  kupiga marufuku mifuko hiyo.

Makamba amesema katazo hilo lina manufaa kwa taifa kàtika kutunza mazingira na kwamba kwa mwaka mifuko bilioni 3 inaishia katika fukwe za mito,bahari na kukaa muda mrefu ikichafua mazingira.
  
Kwaupande wake ,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amewataka watakaopewa mamlaka ya kusimakia katazo hilo kutolichukulia kama fursa ya kuomba na kupokea rushwa.

Kwa baadhi ya mawakala na wafanyabiashara wa mifuko ya plastiki kutoka Sokoni Kariakoo wameiomba serikali iwaongezee muda wa kuiuza hadi Januari mwakani, kwani bado ipo mingi na wanadaiwa na wafanyabiashara raia wa china waliowapa.

Hat hivyo,Waziri Mahakama akijibu hoja hiyo,alisisistiza kuwa katazo hilo ni msimamo  wa Serikali na halitarudi nyuma hivyo wakae na waliowauzia kuona kama watawalipa fidia ama la.


Hivyo makala SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

yaani makala yote SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/serikali-kuandaa-sheriakanuni-katazo-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI"

Post a Comment

Loading...