Loading...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI

Loading...
SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI
link : SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI

soma pia


SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira mazuri Kwa watoto nchini Kwa lengo la kuondoa changamoto wanazokumbana nazo.

Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa ya Themi wakati wa maazimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto yaliofanyika jijini Arusha na kusema kuwa ndio maana serikali ikaanzisha huduma bure ya elimu nchini.

Ameeleza kuwa kumekuwepo na mikakati mbali mbali iliyoandaliwa na serikali Kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na wanaofanyakazi mitaani ikiwa ni lengo la kuwaunganisha na familia zao na jamii kuweza kufikia malengo yao ikiwemo kusoma na kupata matibabu sanjari na makazi.

Awali akimkaribisha mgeni Rasmi Afisa maendeleo ya jamii jiji la Arusha Martha George alisema jiji la Arusha limeweza kuwaunganisha watoto waishio mitaani na mazingira hatarishi katika vituo vya kulea watoto hao na wengine kuwarudisha katika familia zao.

Amesema kuwa malengo ya maadhimisho hayo ya kila mwaka yamejikita kuhakikisha kuona umuhimu wa kuisogeza jamii kuwalea watoto wenye uhitaji na wanaoishi na kufanyakazi mitaani.

Kwa upande wao watoto hao kwenye Risala yao wamesema kuwa wanakumbana na changamoto mbali mbali ikiwemo kutopata elimu sanjari na malezi Bora na kuiomba serikali kuona umuhimu wa kuwaunganisha na familia zao.

Wameeleza kuwa changamoto hizo ni pamoja na jamii kuwanyanyapaa na kuwaona sio sehemu yao Kwa kuwaita majina mbali mbali hivyo kuiomba jamii kuwaona ni sehemu ya maisha yao.

Jumla ya watoto 6,393 Sawa na asilimia 76 wanaishi katika mazingira hatarishi kwenye majiji sita hapa nchini hii imebainishwa na ripoti ya wizara ya afya kwenye mpango wa kizazi kipya Kwa ushirikiano na USAID.

Ambapo watoto wenye umri Kati ya miaka 15-18 Sawa na asilimia 51 huku watoto wenye umri wa miaka 11-14 wakiwa Sawa na asilimia 35 huku ikionyesha watoto wenye umri 0-10 Sawa na asilimia 14 huku watoto wakike wakiwa Sawa na asilimia 86 kwenye umri unaonzia miaka 15-18 

Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi yaliofanyika jijini Arusha yenye kauli mbiu ya "hakikisha usawa Kwa watoto wote" Kwa kuwapatia ulinzi na mahitaji yote Kwa watoto wenye kuishi katika mazingira hatarishi.

Ugumu wa kurudi shuleni uksefu wahali ya upendo vipigo bajeti za watoto wenye kuishi mtaani Kwa kurowabaguza kwani sikuhiini muhimu Kwa kuikumbusha serikali umuhimu wa matunzo ya watotowanaoishi katika mazingira hatarishi.

Jiji la Arusha Lina jumla ya watoto 544 wanaofanyakazi katika kada mbali mbali kama ripori ya serikali inavyoonyesha ambapo watoto hao wanatoa wito Kwa wadau kuwaona kama jamii na kuwasaidia ili nao waje kuwa mfano katika jamii.


Hivyo makala SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI

yaani makala yote SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/serikali-kuendelea-kuboresha-mazingira.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI"

Post a Comment

Loading...