Loading...
title : Tamthiliya Mpya ya Asintado kuoneshwa StarTimes
link : Tamthiliya Mpya ya Asintado kuoneshwa StarTimes
Tamthiliya Mpya ya Asintado kuoneshwa StarTimes
Tamthiliya mpya ya kifilipino, Asintado itaanza kuonyeshwa kupitia StarTiems Novela E Plus jumapili hii tarehe 7. Tamthiliya hii ina hadithi ya “Mahaba na kisasi”. Asintado inakuja baada ya kupokelewa vizuri tamthiliya ya Wildflower ambayo inaisha wikendi hii.
Kila Ijumaa hadi Jumapili, zitakuwa zikionyeshwa sehemu (episode) mbili kuanzia 2:50 kupitia ST Novela E Plus. “Ni kisa cha kuvutia ambacho wapenzi wa tamthiliya wataipenda Asintado. Wahusika wakuu wawili Juliana na Katrina wanaifanya tamthiliya hii kuwa si ya kukosa” Zamaradi Nzowa Meneja Maudhui StarTimes Tanzania
Asintado inawaelezea wasichana wawili, Juliana na Katrina ambao wanatenganishwa na ajali ya moto iliyoharibu nyumba yao na kuwachukua uhai wa wazazi wao, janga hilo likawabadilisha kutoka ndugu hadi maadui wakubwa.Wakati Juliana anaamua kubaki na jina lake, Katrina anabadilisha jina lake na kuwa Samantha Del Mundo. Miaka kadhaa badae wanakutana kipindi ambapo Juliana anaingia kwenye mahusiano na Gael ambaye ni mpenzi wa zamani wa Samantha (Katrina).
Kutokana na wivu, Samantha anatengeneza mpango wa kumuua Juliana, bila kujua kuwa ni ndugu yake waliyepotezana siku nyingi. Kwa bahati mbaya Juliana hakufariki na anataka kulipiza kisasi, anayajenga maisha yake upya na anaapa kummaliza Samantha na wote waliomuumiza.Nini kitatokea baada ya vumbi kutulia na ukweli wote kujulikana? Usikose kuangalia Asintado kuanzia tarehe 7 Aprili. Inapatika katika kifurushi cha Mambo kwa watumiaji wa Antenna na Smart kwa watumiaji wa Dish.
Hivyo makala Tamthiliya Mpya ya Asintado kuoneshwa StarTimes
yaani makala yote Tamthiliya Mpya ya Asintado kuoneshwa StarTimes Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tamthiliya Mpya ya Asintado kuoneshwa StarTimes mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/tamthiliya-mpya-ya-asintado-kuoneshwa.html
0 Response to "Tamthiliya Mpya ya Asintado kuoneshwa StarTimes"
Post a Comment