Loading...

TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI

Loading...
TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI
link : TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI

soma pia


TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinwumi Adesina, Mjini Washington DC, Marekani, kabla ya mkutano wa magavana wa Benki hiyo ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54 zenye hisa kwenye benki uliofanyika katika ukumbi wa Willard Continental kujadili namna ya benki hiyo kuongezewa mtaji ili iweze kutoa mikopo kwenye nchi hizo kwa ufanisi zaidi
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango  akifuatilia kwa makini mjadala wa namna Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB inavyoweza kuongezewa mtaji, Mjini Washington DC, Marekani, ambapo Tanzania imeridhia hatua hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akifuatilia kwa makini mjadala wa namna Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, inavyoweza kuongezewa mtaji, Mjini Washington DC, Marekani, ambapo Tanzania imeridhia hatua hiyo
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Washington DC
Na.Benny Mwaipaja, WFM, Washington DC
TANZANIA imeunga mkono uamuzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB wa kutaka kuongezewa mtaji ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa mikopo kwa nchi wanachama wa benki hiyo kwa lengo la kuchochea zaidi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano wa 7 wa magavana wa ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54  wanachama wa Benki hiyo, Mjini Washington DC, Marekani, Waziri wa Fedfha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameeleza kuwa AfDB imefanya mambo makubwa nchini Tanzania ndio sababu inaunga mkono kusudio hilo.
Amesema kuwa Benki hiyo imeipatia Tanzania mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, kilimo, nishati na maji.
Benki inataka kuongezewa mtaji kwa asilimia 200 kutoka wastani wa UA bilioni 67.69 hadi UA 191.89 (kutoka dola za Marekani 94.76 hadi dola bilioni 268.6 ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii ya nchi wanachama hususan katika ujenzi wa reli, barabara, usafiri wa anga, tehama, bandari, uzalishaji na usambazaji wa nishati.
"Wakati umefika ili twende haraka zaidi, mitaji sehemu nyingine imepungua, pendekezo la kuongeza mtaji wa benki hii ni jema na matokeo ya miradi inayofadhiliwa na Benki hii yanaonekana katika nchi zetu za kiafrika kwa sababu benki hii iko Afrika na inaijua Afrika tofauti na benki nyingine" alisisitiza Dkt. Mpango
Uamuzi wa nchi za Kiafrika zenye hisa katika Benki ya Maendeleo ya Afrika ya kutaka Benki hiyo iongezewe mtaji ulitolewa wakati wa mkutano wa Magavana wa Benki hiyo mjini Rome, Italia, baada ya mahitaji ya nchi wanachama ya kutafuta mikopo kwenye taasisi hiyo kuongezeka.


Hivyo makala TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI

yaani makala yote TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/tanzania-yaridhia-benki-ya-maendeleo-ya_14.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI"

Post a Comment

Loading...