Loading...
title : TASWA YAKAMILISHA HATUA MUHIMU KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA
link : TASWA YAKAMILISHA HATUA MUHIMU KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA
TASWA YAKAMILISHA HATUA MUHIMU KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA
KAMATI ya Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) imekamilisha hatua zote muhimu kuhusu marekebisho ya katiba hiyo na sasa imeitisha mkutano wa wadau wote Aprili 12 mwaka huu kwa ajili ya kuijadili na kuipitisha rasimu hiyo.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Kamati ya Katiba ya TASWA inaamini mkutano huo utakuwa na tija katika kuboresha rasimu hiyo ili taratibu zingine ziendelee ikiwa ni pamoja na kupanga tarehe ya uchaguzi wa TASWA.
Kwa vile Kamati imekamilisha jukumu ililopewa la kuandaa rasimu hiyo, hivyo kilichobaki ni ushirikiano kutoa kwa wadau ili kumaliza jambo hilo.
Pamoja na mambo mengine rasimu hiyo imeandaliwa kwa kuangalia Katiba za vyama mbalimbali duniani vinavyohusiana na waandishi wa habari za michezo na pia kupitia muongozo kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), ambacho TASWA ni mwanachama.
Pia Kamati imechambua Katiba ya sasa ya TASWA na kupokea maoni kutoka kwa waandishi wa habari za michezo kuhusu maeneo yenye upungufu kwa nia ya kuiboresha.
Maeneo mbalimbali yamefanyiwa kazi katika rasimu hiyo baadhi yakiwa ni sifa ya mwanachama, wajibu wa mwanachama, muundo wa uongozi, sifa za viongozi na pia ukomo wa uongozi. Pia kuna mapendekezo katika rasimu hiyo ya kuanzishwa kamati mbalimbali kwa nia ya kuisaidia Kamati ya Utendaji.
Kamati ya Katiba ya TASWA imeundwa kutokana na agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliyeitaka BMT isitishe uchaguzi wa TASWA uliokuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana na badala yake BMT ikutane na viongozi wa TASWA pamoja na baadhi ya wanahabari wa michezo kuona namna ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TASWA iendane na wakati.
Kamati ya Katiba inayoongozwa na Mwenyeketi wa zamani wa TASWA, Boniface Wambura ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), viongozi wengine ni Katibu wa Kamati Amir Mhando ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TASWA na mwanahabari, Gift Macha ambaye ni Katibu Msaidizi wa Kamati.
Wajumbe ni Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Abdul Mohammed, Mhazini wa zamani wa TASWA, Nasongelya Kilyinga na wanahabari Thabit Zacharia na Devotha Kihwelu.
Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu wa Kamati ya Katiba/ Katibu Mkuu TASWA
5/04/2019
Hivyo makala TASWA YAKAMILISHA HATUA MUHIMU KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA
yaani makala yote TASWA YAKAMILISHA HATUA MUHIMU KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TASWA YAKAMILISHA HATUA MUHIMU KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/taswa-yakamilisha-hatua-muhimu-kuhusu.html

0 Response to "TASWA YAKAMILISHA HATUA MUHIMU KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA"
Post a Comment