Loading...

TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI

Loading...
TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI
link : TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI

soma pia


TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marukufu kuuzwa kwa nyaya za kupitia mawasiliano (Data Cable) zilizokuwa zikiuzwa kwenye baadhi ya maduka ya vifaa vya kielektroki baada ya kubainika hazikidhi viwango.

Hatua hiyo ilifikiwa na maofisa wa shirika hilo kwenye baadhi ya maduka jijini Dar es Salaam baada ya sampuli za nyaya hizo kupimwa kwenye maabara na kudhibitika hazikidhi viwango.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mkaguzi wa TBS, Saimon Emmanuel, amesema tayari wenye maduka yaliyokuwa yakiuza nyaya hizo wamepewa muda wa siku 14 kujieleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua.

Amesema baada ya kujiridhisha kuwa nyaya hizo hazikidhi viwango, hatua ya kwanza iliyochukuliwa ni kuzuia nyaya hizo kuendelea kuuzwa na ametoa mwito kwa Watanzania kutozinunua na kigezo kimoja wapo wanachoweza kutumia kuzitambua ni kuuzwa bei ndogo.

Pia amesema baada ya kupimwa kwenye maabara za shirika pamoja na kasoro nyingine, nyaya hizo zilibainika kuwa na kiwango kidogo cha madini ya shaba (copper) na kwamba hata nguvu kinzani kwenye nyaya hizo zilifeli kwenye maabara .

"Hivyo tumezizuia kwenye maduka tukisubiri hatua nyingine," amesema na kutoa mwito kwa wafanyabiashara wanapotaka kununua bidhaa kutoka nje ya nchi kuhakikisha zinakaguliwa ubora wake nje ya nchi kabla hazijaingia nchini mpangao ambao kitaalamu unaojulikana kama kama Pre-Shipment/Export Verification of Conformity to Standards (PVoC).

Pia ameongeza kuws wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi bila kukabuliwa kupitia PVoC, pindi bidhaa zao zinapofika nchini wanatozwa faini ya asilimia 15 kulingana na thamani ya mzigo, kulipia gharama za upimaji kwenye maabara na kwamba zinapofeli kufikia viwango muagizaji anaamuriwa kuzirudisha alikozitoa kwa gharama zake au kuteketezwa hapa nchini pia kwa gharama zake.

Emmanuel amesema hiyo ni kwa mujibu wa Sheria Na:2 ya Viwango ya mwaka 2009. Ametoa mwito kwa wafanyabiashara kuhakikisha wazingatia sheria na taratibu ili kuepuka hasara.

Shirika hilo kwa sasa linaendesha awamu ya pili ya msako wa kushtukiza wa bidhaa zilizopo sokoni ili kubaini bidhaa ambazo hazina ubora na kuziondoa kwenye soko.



Hivyo makala TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI

yaani makala yote TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/tbs-yazuia-uuzwaji-nyaya-za-mawasiliano.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TBS YAZUIA UUZWAJI NYAYA ZA MAWASILIANO KATIKA MADUKA YA VIFAA VYA KIELETRONIKI"

Post a Comment

Loading...