Loading...
title : TCRA: Changamoto Vitambulisho vya Taifa itatatuliwa na Mamlaka husika sambamba na zoezi la Usajili
link : TCRA: Changamoto Vitambulisho vya Taifa itatatuliwa na Mamlaka husika sambamba na zoezi la Usajili
TCRA: Changamoto Vitambulisho vya Taifa itatatuliwa na Mamlaka husika sambamba na zoezi la Usajili
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV, Morogoro
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya mashariki imesema kuwa changamoto ya wananchi kukosa vitambulisho vya Taifa kwa ajili ya kusajili namba za simu kwa kutumia namba za vidole itatatuliwa na Mamlaka inayotoa vitambulisho hivyo (NIDA).
Changamoto ya vitambulisho hivyo imeibuka wakati Kanda ya Mashariki ilipokuwa inatoa elimu maeneo mbalimbali ya mkoani Morogoro kwa wananchi kuhoji vitambulisho vya taifa namna ambapo watavipata kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya mashariki imesema kuwa changamoto ya wananchi kukosa vitambulisho vya Taifa kwa ajili ya kusajili namba za simu kwa kutumia namba za vidole itatatuliwa na Mamlaka inayotoa vitambulisho hivyo (NIDA).
Changamoto ya vitambulisho hivyo imeibuka wakati Kanda ya Mashariki ilipokuwa inatoa elimu maeneo mbalimbali ya mkoani Morogoro kwa wananchi kuhoji vitambulisho vya taifa namna ambapo watavipata kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa muda uliowekwa kwa ajili ya usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole unafanya kila mwananchi atapata kitambulisho cha Taifa na kuweza kusajili laini kwa kutumia alama za vidole.
Aidha amesema kuwa baadhi ya watu walikuwa wanatumia simu ambazo zimesajiliwa na kwa majina ya watu wengine ambapo ni kosa kisheria. Amesema kuwa usajili wa laini kwa alama za vidole inaondoa mtu kumiliki laini kwa jina la mtu mwingine. Amesema kuwa katika kipindi hiki cha usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole kwa wenye vitambulisho wajisajili na wasiokuwa navyo wafuate utaratibu kwa kuvipata katika mamlaka husika kuweza kuvipata kwani mwisho wa kusajili ni Desemba 31 mwaka huu ambapo wasiosajili simu zao zitafungiwa.
Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Robson Shaban akimpa maelezo mwananchi wa kijiji cha Mkuyuni.
Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Christopher John akitoa maelezo namna kutumia mawasiliano na umuhimu wa kusajili laini kwa kutumia alama za vidole wakati kanda hiyo ilivyokwenda kutoa elimu katika kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro.
Wananchi wakipata elimu ya mawasiliano pamoja na usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole katika mnada wa kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wananchi wa Mkuyuni Mkoani Morogoro katika mnada wa kijiji hicho walipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano na Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole
Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Violet Eseko akitoa maelezo ya kisheria ya kumiliki simu zisizokuwa na majina yao wakati wa utoaji wa elimu kwa wananchi Mkuyuni mkoani Morogoro.
Mwananchi wa kijiji cha Mkuyuni akiuliza swali kwa TCRA Kanda ya Mashariki ilipokwenda kutoa elimu katika kijiji hicho.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na Abood Tv mara baada ya kumaliza kipindi cha utoaji elimu katika Radio Abood mkoani Morogoro
Hivyo makala TCRA: Changamoto Vitambulisho vya Taifa itatatuliwa na Mamlaka husika sambamba na zoezi la Usajili
yaani makala yote TCRA: Changamoto Vitambulisho vya Taifa itatatuliwa na Mamlaka husika sambamba na zoezi la Usajili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCRA: Changamoto Vitambulisho vya Taifa itatatuliwa na Mamlaka husika sambamba na zoezi la Usajili mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/tcra-changamoto-vitambulisho-vya-taifa.html
0 Response to "TCRA: Changamoto Vitambulisho vya Taifa itatatuliwa na Mamlaka husika sambamba na zoezi la Usajili"
Post a Comment