Loading...
title : TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
link : TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
VICTOR MASANGU, KIBAHA
VIJANA wapatao 35 katika halmashauri ya mji Kibaha iliyopo Mkoani Pwani ambao walikuwa wanakabiliwa na wimbi la ukosefu wa upatikanaji wa ajira wamepatiwa mafunzo maalumu ya ujasiriamali kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na tatizo la umasikini.
Hayo wamebainishwa na Meneja wa Taasisi ya ujasiramali na ushindani Tanzania (TECC) Anna Manuti wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku 11 ya ujasiliamali kwa baadhi ya vijana waliopo katika halmashauri ya mji Kibaha ambayo yameandaliwa kwa lengo la kuwapa mbinu mbali mbali zitakazoweza kuwasaidia kujiajiri na kuacha na kuwa tegemezi.
Aidha Meneja huyo amebainisha kuwa katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili baadhi ya vijana wameamua kuwakutanisha vijana hao kwa lengo la kuwawezesha kwa kuwapatia elimu ambayo itawapa fursa ya kuanzisha biashara zao wenyewe lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
“Hii programu ya kuwawezesha vijana mafunzo ya ujasiriamali tunaifanya kwa kipindi cha miaka miaka mine na inatarajia kumalizika mwaka 2020 na kwa sasa huu ni mzunguko wa sita ambapo katika halmashauri ya mji wa kibaha vijana wapatao 35 wamepata fursa ya kupatiwa mafunzo haya ambayo yatawea kuwasaidia kuweza kujiajiri wao wenyewe,”alisema Anna.
Kwa upande wake Meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Behata Minga amesema programu ya kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali itawasaidia vijana kujiajiri wao wenyewe kutokana kuanzisha viwanda vidogovidogo lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi na kupambana na wimbi la umasikini.
“Kwa kweli mradi huu wa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana hasa katika Mkoa wetu wa Pwani na sisis kama Sido tutahakikisha tunashirikiana bega kwa beda na taasisi hii ya TECC ambayo imefanikisha kuwakusanya vijana hawa na kuwapa mahalifa ambayo yatawasaidia kupata ajira pamoja na kuanzisha viwanda vidogividogo,”alisema Mlinga.
Nao baadhi ya vijana ambao wameshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Selemani Shabani pamoja na Azaria Namga wamesema kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na ajira, ukosefu wa mitaji ya biashara hivyo wameiomba serikali ya awamu yatano kuwasaidia kwa halina mali ili kufanikisha malengo waliyojiwekea.
MRADI huo wa kuwawezesha vijana kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali unatekelezwa katika mikoa mine ya Jiji la Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara pamoja na Pwani ambapo hadi sasa katika mikoa yote hiyo vijana wapatao 894 wamenufaika na programu hiyo ambayo inatarajia kumalizika mwaka 2020.
Hivyo makala TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
yaani makala yote TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/tecc-yatoa-mafunzo-ya-ujasiriamali-kwa.html
0 Response to "TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI"
Post a Comment