Loading...
title : TRC YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU TRENI YA UMEME
link : TRC YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU TRENI YA UMEME
TRC YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU TRENI YA UMEME
SHIRIKA la reli nchini limewatoa hofu watanzania kuhusu umeme Utakao tumika katika shughuli zote za kuendesha usafiri wa treni ya umeme inayotarajiwa kuanza kazi zake za usafiri tokea Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa hatua ya kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa mradi kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro Eng Ayubu Mdachi alisema kuwa kukamilika kwa reli hiyo kutaongeza pato kubwa kwa taifa.
Aidha amewataka wananchi kuwa walinzi wakuu wa mradi huo kwani kuna watu wengine hawana nia njema na maendeleo ya nchi yetu.
Aliongeza kuwa umeme utakaotumika katika uendeshaji wa treni hiyo ni wa hali ya juu kwani kila mkoa utakuwa umeunganishwa hivyo kama ikitokea kukatika kwa umeme Morogoro basi treni hiyo itatumia wa mkoa wa pwani la sivyo ukatike nchini nzima napo bado treni hiyo itafanya kazi zake kutokana na uwezo wake wa kutunza umeme yenyewe.
Kwa upande wake Edwini Kalisa katibu wa baraza la wafanyakazi la shirika la reli nchini alisema kuwa serikali inasitahili pongezi za dhati kutokana na hali halisi jinsi inavyoelekea katika nchini yetu kwani mizigo itasafirishwa kwa urahisi na haraka kuliko Barabara za kupitia magari.
Aliongeza kuwa usafirishaji wa treni ijayo ya umeme itasaidia sana kwenye sekta ya viwanda kutokana na uwepo wa malighafi kutegemeana kutoka sehemu mbalimbali za mkoa.
Aidha katibu huyo aliongeza kuwa treni hiyo itakuwa ni ya kwanza barani Afrika kutokana na ubora wake unavyoonekana.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la reli nchini,Edwini Kalisa akizungumza leo na waandishi wa habari katika kituo cha soga mara baada ya kutembelea na kukagua jinsi mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa standard Gauge Soga mkoa Pwani.(Picha na Emmanule Massaka wa Mchuzi TV Dar es Salaam)
Meneja Msaidizi SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC), Mhandisi,Ayubu Mdachi, akizungumza na wafanyakazi la shirika la reli nchini namna mradi huo unavyoendelea katika Lot 1 inayotoka Dar es Salaam mpaka Morogoro.
wafanyakazi la shirika la reli nchini wakiangalia reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga mkoa wa Pwani.
Picha ya pamoja
Hivyo makala TRC YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU TRENI YA UMEME
yaani makala yote TRC YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU TRENI YA UMEME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRC YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU TRENI YA UMEME mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/trc-yawatoa-hofu-watanzania-kuhusu.html
0 Response to "TRC YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU TRENI YA UMEME"
Post a Comment