Loading...
title : UCHAGUZI WA KIHISTORIA KUSHUHUDIWA NCHINI INDIA, WATU MILIONI 900 KUPIGA KURA
link : UCHAGUZI WA KIHISTORIA KUSHUHUDIWA NCHINI INDIA, WATU MILIONI 900 KUPIGA KURA
UCHAGUZI WA KIHISTORIA KUSHUHUDIWA NCHINI INDIA, WATU MILIONI 900 KUPIGA KURA
* Watu milioni 900 wakiwemo vijana wajiandikisha kupiga kura, siku 38 zatengwa kwa kupiga kura
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
INDIA ina wapiga kura takribani Milioni 900(Ni Mara 18 zaidi ya Idadi ya watanzania wote) waliojiandikisha kwenye Time ya Uchaguzi.
Zoezi la kupiga kura litaanza tarehe 11 April hadi tarehe 19 Mei 2019, yaani takribani siku 38 kwa mizunguko 7 na kisha kura zitaanza kuhesabiwa tarehe 23 Mei 2019.
Waziri Mkuu wa sasa, Narendra Modi na chama chake cha BJP amerudi tena na kuomba kutetea tena kiti hicho.
Akizungumza na vyombo vya habari msemaji wa tume ya uchaguzi nchini humo, Sunil Arora, amesema kuwa uchaguzi utafanyika Aprili 11, mwaka huu na utawahusisha wapigakura milioni 900 na kati yao wapiga kura milioni 15 ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 19.
Katika kipindi cha wiki chache zilizopita, tatizo la uhaba wa ajira na kushuka kwa bei ya bidhaa za kilimo, vilishusha umaarufu wa Waziri Mkuu Modi, lakini wapigakura wanasema Chama Tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP), kitawapiku wapinzani wake baada ya mwezi uliopita jeshi la polisi la nchi hiyo kuingia vitani na wapinzani wa Pakistan hali inayoelezwa imewapa umaarufu zaidi na kuweza kupelekea kujizolea mamilioni ya kura kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Hivyo makala UCHAGUZI WA KIHISTORIA KUSHUHUDIWA NCHINI INDIA, WATU MILIONI 900 KUPIGA KURA
yaani makala yote UCHAGUZI WA KIHISTORIA KUSHUHUDIWA NCHINI INDIA, WATU MILIONI 900 KUPIGA KURA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UCHAGUZI WA KIHISTORIA KUSHUHUDIWA NCHINI INDIA, WATU MILIONI 900 KUPIGA KURA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/uchaguzi-wa-kihistoria-kushuhudiwa.html
0 Response to "UCHAGUZI WA KIHISTORIA KUSHUHUDIWA NCHINI INDIA, WATU MILIONI 900 KUPIGA KURA"
Post a Comment