Loading...

Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera

Loading...
Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera
link : Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera

soma pia


Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera

 Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe.Selemani Mzee akifungua kikao kazi cha kupokea rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka jana mjini Masasi
 Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Edwin Mgendera akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu rasimu ya sera mpya ya madaraka kwa umma jana mjini Masasi.
 Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha kupokea maoni ya rasimu ya taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambao ni Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Weenyeviti wa Halmashauri, wabunge, na viongozi wa asasi za kiraia kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma wakishiriki kikao hicho mjini Masasi jana.


Na Mathew Kwembe, Masasi 

Serikali imesema Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ya mwaka 2019 ambayo hivi sasa ipo katika hatua ya rasimu itakapokamilika itakuwa na nguvu ya kisheria na kisera tofauti na ile ya mwaka 1998 ambayo ilikuwa ni sera ambayo haikuwa na nguvu ya kisheria. 

Hayo yameelezwa jana mjini Masasi, mkoani Mtwara na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Kisheria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Edwin Mgendera mara baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau juu ya rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka ya mwaka 2019 kwa wananchi wa mikoa ya kusini ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. 

Bwana Mgendera amesema mafanikio na changamoto zilizotokana na utekelezaji wa Sera ya Ugatuaji ya mwaka 1998 imeiwezesha serikali kuja na Sera ya jumla ya ugatuaji kitaifa ambayo itakuwa na nguvu za kisheria na namna bora ya kutekeleza na kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi toka juu serikalini hadi ngazi za chini za Kitongoji na Mtaa kule kwenye Halmashauri. 

Amesema mwelekeo wa serikali kwa sasa ni huo wa kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambayo itawekewa nguvu za kisheria na kisera ili kurahisisha suala la utoaji huduma kwa wananchi moja kwa moja kutoka serikali kuu hadi ngazi za kitongoji na mtaa. 

Mkurugenzi huyo wa huduma za Sheria amefafanua kuwa Msingi wa Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka, 1977 Ibara ya 145 na 146 ambazo zimetoa uhalali wa kuanzishwa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kubainisha madhumuni ya kuanzishwa kwa Mamlaka hizo yakiwemo kuzipa Mamlaka za Serikali za Mitaa madaraka ya kujiamulia mambo yao ya Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi katika maeneo yao kwa uhuru. 

“Aidha Sheria Na. 7 ya Halmashauri za Wilaya ya mwaka 1982 (sura 287) na Sheria Na. 8 ya Halmashauri za Miji ya mwaka 1982 (sura 288) zinazipa mamlaka hizo majukumu ya kutoa huduma kwa jamii katika maeneo husika,” amefafanua bwana Mgendera. 

Pia Mkurugenzi huyo ameitaja sheria ya Tawala za Mikoa ya Mwaka 1997 ambayo inazipa Tawala za Mikoa jukumu la kuratibu maendeleo katika Mikoa yao ikiwemo kuzisimamia na kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa huduma bora kwa usawa kwa jamii. 

Ni kutokana na msingi huo wa sheria bwana Mgendera amesema kuwa masuala ya Ugatuaji wa Madaraka yanafanyika na yataeendelea kufanyika katika hatua mbili muhimu ambazo ni kugatua Madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda Ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji) na pili kugatua Madaraka kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenda ngazi za Msingi yaani Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Kisekta kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Juma Idd ambaye pia ndiye Mratibu wa kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau juu ya rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka ya mwaka 2019 ameeleza kuwa hivi sasa timu yake ipo katika mikoa hiyo ya kusini baada ya zoezi hilo kukamilika katika mikoa ya nyanda za juu kusini ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa. 

Ameongeza kuwa baada ya kukamilika katika mikoa hiyo, timu ya kupokea maoni itaelekea katika kanda ya mashariki ambapo Mikoa ya Morogoro, Dar es salaam, Pwani na Dodoma itashirikishwa, na baadaye zoezi hilo kuhamia mikoa ya kaskazini, magharibi na kanda ya ziwa. 

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa wadau wetu muhimu wanapata fursa ya kutoa maoni yao juu ya nini wangependa kiwemo katika sera yetu hii mpya ya Ugatuaji wa Madaraka,” amesema bwana Idd. 

Awali akifungua kikao kazi cha kupokea maoni Mkuu wa Wilaya ya Masasi bwana Selemani Mzee ameeleza umuhimu kikao hicho ambapo amesema kuwa toka mwaka 1998 Serikali kupitia Rasimu ya maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) imekuwa ikitekeleza dhana ya ugatuaji wa Madaraka ili kufikisha na kuharakisha utoaji wa huduma za Kijami,Kiutawala na Kiuchumi kwa wananchi kwa haraka na kwa usawa. 

Amesema kuwa kupitia dhana ya ugatuaji wa madaraka, wananchi wanapata fursa ya kutosha ya kushiriki na kushirikishwa katika shughuli na masuala yote yanayohusu maendeleo yao na ustawi wa maisha yao. 

Miongoni mwa wanaoshiriki kikao hicho ni pamoja na waheshimiwa Wabunge wanaotoka Mikoa ya kusini ambapo Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mheshimiwa Hassan Elias Masala amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwao kama wawakilishi wa wananchi kwani utekelezaji wa ahadi nyingi za serikali kupitia chama kilichopo madarakani hivi sasa unategemea sana utekelezaji wa sera hii ya ugatuaji wa madaraka. 

Naye Bi Miriam Mwaibula mshiriki kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA amesema kuwa maoni yao ni muhimu kwani yatawezesha serikali kupata sera madhubuti na ambayo itakubalika na jamii yote na hivyo kurahisisha utekelezaji wake. 

Kikao hicho cha siku mbili kimewahusisha Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi kutoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa dini na Washiriki kutoka Asasi za Kiraia kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma. 


Hivyo makala Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera

yaani makala yote Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/ugatuaji-wa-madaraka-sasa-kuwa-na-nguvu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera"

Post a Comment

Loading...