Loading...
title : ULEGA AWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MVUA NA KUSABABISA NYUMBA ZAO KUBOMOKA
link : ULEGA AWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MVUA NA KUSABABISA NYUMBA ZAO KUBOMOKA
ULEGA AWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MVUA NA KUSABABISA NYUMBA ZAO KUBOMOKA
Na Shushu Joel,Mkuranga.
Akizungumza na wananchi hao Ulega aliwapa pole na kuwaomba kuendelea kuwa na subra wakati serikali ya awamu ya tano ikifanya tathimini ili kubaini kaya zote zilizokumbwa na majanga hayo.
Aliongeza kuwa majanga kama haya si ya kisiasa bali yanapangwa na Mungu hivyo katika kipindi hiki kigumu kwa wananchi wa vikindu ambao ndio waathirika wakubwa wanapaswa kuendelea kuwa watulivu.
Aidha alisema kuwa taarifa za awali alizozipata kuhusu kaya zilizokumbwa na majanga hayo zilikuwa ni 100 lakini kufikia jioni ziliongezeka mpaka kufikia kaya 178 ,ni kaya nyingi kwa kweli kwani wananchi hao wanapata changamoto kwa sasa.
Pia Naibu waziri huyo amewapatia pole wananchi hao zilizotolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kusema anatambua kilichotokea katika jimbo la Mkuranga na kuwataka kuzidisha maombi ili Mungu awaondolee majanga.
Aidha katika ziara hiyo ya kuwatembelea wahanga hao Ulega ametembelea familia iliyopoteza mama na mtoto kwa kuuwawa kwa radi.
"Ofisi ya mbunge imetoa kiasi cha zaidi ya milioni 3 ili kusaidia baadhi ya wahanga wa nyumba zilizoezuliwa na upepo mkali na itaendelea kuwasaidia ili kuhakikisha kila mmoja anarudi kwenye nyumba yake na kuendelea na shughuli zake za uzalishaji"Alisema Ulega.
Kwa upande wake shuhuda wa tukio hilo,Juma Said alisema kuwa radi iliposhuka katika maeneo hayo hali ya hewa kama ilibadirika yote mama wa familia hiyo alikuwa nje ghafla alianguka na huku vijana waliokuwa ndani walipiga kelele ndio tuliwai kutoa msaada kwa mama huyo kimkimbiza hospital ila kijana alikuwa ameshakwisha kufariki.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega akiwapa pole wanafamilia waliokumbwa na majanga ya kubomoka kwa nyumba zao na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega akiwapa pole wanafamilia waliokumbwa na majanga ya kubomoka kwa nyumba zao na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega kulia akiwa amekaa na wafiwa katika msiba , ambapo aliwafariki na kuwaomba kuendelea kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu ,Wananchi wa vikindu ambao ndio waathirika wakubwa wanapaswa kuendelea kuwa watulivu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega akimsikiliza mmoja wa wananchi ambae nyumba yake ilikumbwa na majanga ya kubomoka na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Hivyo makala ULEGA AWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MVUA NA KUSABABISA NYUMBA ZAO KUBOMOKA
yaani makala yote ULEGA AWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MVUA NA KUSABABISA NYUMBA ZAO KUBOMOKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ULEGA AWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MVUA NA KUSABABISA NYUMBA ZAO KUBOMOKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/ulega-awafariji-walioathiriwa-na-mvua.html
0 Response to "ULEGA AWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MVUA NA KUSABABISA NYUMBA ZAO KUBOMOKA"
Post a Comment