Loading...
title : UNAIKUMBUKA BEMBEYA JAZZ YA GUINEA?
link : UNAIKUMBUKA BEMBEYA JAZZ YA GUINEA?
UNAIKUMBUKA BEMBEYA JAZZ YA GUINEA?
Na Moshy Kiyungi
Miaka ya nyuma palikuwa na wimbo wa Whsky Soda, uliojizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa wapenda muziki katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati. Wimbo huo ulipokuwa ukipigwa katika radio yeyote, watu walikuwa wakiufurahia kusikia sauti ya maneno yasiyo eleweka ya ‘Chapombe’, neno la “ila Whsky Soda”.
Wimbo huo uliopigwa katika mtindo wa aina yake, ni kazi nzuri ya bendi Bembeya Jazz toka nchini Guinea, ambayo hutajwa kama ni nguzo ya historia ya muziki wa kisasa wa Afrika Magharibi. Mwaka 1958 kulikuweko na kura ya maoni katika nchi zilizotawaliwa na Wafaransa huko Afrika Magharibi, ambapo wananchi waliulizwa kama wanataka kuendelea kuwa chini ya Ufaransa. Nchi ya Guinea ndio pekee iliyokataa.
Ahmed Sekou Toure akachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, na kati ya vitu alivyoanzisha mara moja ilikuwa ni Bendi ya Taifa iliyoitwa Syli National Orchestra. Bendi hiyo ilikuwa na maskani katika jiji la Conakry, iliendelea kukua hatimae mwaka 1961, ikagawanyika katika makundi mawili ya Bala et ses Balladins na Keletigui et Ses Tambourinis.
Kutokana na upenzi wake wa sanaa, rais Sekou Toure alitengeneza bendi za mikoani, ambazo alizifadhili kwa vyombo na fedha. Katika jiji la Beyla Kusini Mashariki mwa Guinea kwenye mwaka 1961, Gavana wa mkoa huo Emile Conde alianzisha kakundi kake kadogo kakiwa na gitaa moja tu kavu. Pasipo uzoefu mwingi lakini taratibu kakanza kujitokeza mbele ya jamii.
Kabendi hako toka mikoani, kalishinda mashindano mengi na kujulikana sana mjini Conakry. Hatimae Chama tawala kiliitaka bendi ya Bembeya ihamie Conakry mwaka 1965. Kabendi hako kakataifishwa na kufanywa bendi ya Taifa kama zile nyingine mbili.
Bendi hii ilianza kwa kuitwa Beyla Jazz, lakini siku moja April 1961, katika mkutano wa bendi wakaamua kujiita Bembeya Jazz. Wakati huo Guinea kulikuwa na aina mbili za wanamuziki wale waliopiga muziki wao wa asili na wale waliotoka kwenye shule za Kifaranza amabo walipiga muziki wa asili ya Cuba.
Amri ilitolewa na serikali kuelekeza wanamuziki wapige muziki kutokana na vionjo vya kwao katikati ya miaka ya 1960. Hivyo ukisikia nyimbo za Bembeya Jazz kabla ya hapo unasikia vionjo vya Cuba kama zile za Whisky Soda na Mamiwata, ni mfano wa upigaji huo. Baada ya hapo mpaka ilipokuja kurekodi mara ya mwisho bendi hiyo imekuwa na vionjo vya muziki wa asili wa Guinea.
Wakati wa uhai wa Sekou Toure, nchi hiyo ilianzisha nembo ya kurekodia iliyoitwa Syliphone. Ilikuwa ni nembo ya Taifa, jambo hilo halikuwahi kufanyika popote Afrika. Tanzania ilijaribu kuiga mfumo huo na iliweza kutoa kazi chache kwa kutumia Kampuni ya Filamu Tanzania na kuwa na nembo za TFC na Sindimba.
Uchumi wa nchi ya Guinea iliporomoka mnamo miaka ya 1970. Nembo hiyo iliweza kutoa album 80 na ikawa ndiyo mwisho wa bendi hiyo. Kufuatia hali ya Uchumi kuwa mbaya, baadhi ya wanamuziki wa nchi hiyo wakaanza kuelekea nchini ya Ufaransa na nyingine kujitafutia maisha. Yaelezwa kwamba rais Sekou Toure alifanya kazi kubwa kwa nchi yake kwa upande wa sanaa na kuweza kuifanya Guinea kuwa kati ya nchi zilizoongoza Afrika katika utamaduni wa muziki.
Kila kizuri hakikosi kasoro. Rais huyo taratibu akaanza kufanya udikteta mkubwa kwa watu waliompinga. Kila aliyefanya hivyo alipotea au kuuawa.
Kama ilivyotokea kwa Fodeba Keita msanii aliyeanzisha kundi la kwanza la Ballet nchini Guinea, rais Sekou Toure akamfanya Waziri wa Mambo ya Ndani, lakini kufikia mwishoni mwa miaka ya 1960, rais huyo akawa na wasiwasi wa kupinduliwa na Fodeba.
Kwa mamlaka aliyokuwa nayo, alimfunga na hatimae Fodeba akapotea wala haikujulikana alikufa vipi au lini. Pamoja na udikteta huo alikuwa tofauti na ule wa aliyekuwa rais wa Zaire sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mobutu Seseseko. Rais Toure alikuwa mzalendo hakuwa fisadi wa kuiba mabilioni na kuyatorosha nje, ila aligeuka akawa katili kwa kulinda himaya ya utawala wake.
Pamoja na maelfu ya Waguinea kuikimbia nchi yao kutokana na utawala huo, Wanamuziki wachache walimlaani, wengine walifaidika na fadhila zake katika tasnia ya muziki. Kufikia mwaka 1980 Bembeya Jazz ilikuwa haipigi tena maonyesho ya kawaida labda kwa kukodishwa.
Kati ya mambo makubwa ya kusikitisha yaliyo kikumba kikundi hicho ni kifo cha muimbaji wao Demba Camara, aliyefariki katika ajali ya gari lao lililokuwa likiendeshwa na dereva wa bendi yao ilipopinduka wakiwa safarini. Katika gari hilo pia alikuweko Sekou 'Bembeya' Diabate (Diamond Finger).
Demba alikutwa ametupwa nje ya gari, walipowasili wanamuziki wengine waliokuwa katika gari jingine. Mwanamuziki Sekou 'Bembeya' Diabate, bado anafanya maonesho lakini hasa nje ya Guinea. Hakuna ubishi kuwa historia ya sanaa ya Tanzania, iliiga baadhi ya taratibu za sanaa za rais Sekou Toure wa Guinea, kwa kuanzishwa kwa kundi la Sanaa la Taifa.
Si hivyo tu kwani kulianzishwa bendi ya Wanawake, iliyotokana na ziara za rais huyo hapa kwetu. Yeye alikuja kasindikizana na kundi kubwa la wasanii wa kundi la Taifa.
Hivyo makala UNAIKUMBUKA BEMBEYA JAZZ YA GUINEA?
yaani makala yote UNAIKUMBUKA BEMBEYA JAZZ YA GUINEA? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UNAIKUMBUKA BEMBEYA JAZZ YA GUINEA? mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/unaikumbuka-bembeya-jazz-ya-guinea.html
0 Response to "UNAIKUMBUKA BEMBEYA JAZZ YA GUINEA?"
Post a Comment