Loading...
title : WANARIADHA MASHUHURI KUSHIRIKI NGORONGORO MARATHONI APRIL 20
link : WANARIADHA MASHUHURI KUSHIRIKI NGORONGORO MARATHONI APRIL 20
WANARIADHA MASHUHURI KUSHIRIKI NGORONGORO MARATHONI APRIL 20
Na woinde shizza globu ya jamii Arusha
Wanariadha nyota wa Tanzania Alfonce Simbu na Josephy Panga ni miongoni mwa wakimbiaji mashuhuri ambao watashiriki katika mashindano ya Ngorongoro marathon yanayotarajiwa kufanyika April 20 mwaka huu.
Wakimbiaji wengine nyota waliothibitisha kushiriki mashindano ni pamoja na Failuna Matanga,Anjelina Tsere ,Magdalena Shauri ,Fabian Joseph ,Faraja Damas pamoja na Natalia Elsante.
Akizungumza na Globbu ya Jamii leo muandaaji wa mbio hizo Meta Petro alisema kuwa mbio hizi ambazo zinafanyika kwa miaka 12 mfululizo zitashirikisha wakimbiaji zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji mashuhuri kutoka nchini Kenya.
Alisema mbio hizo zitakuwa za kilometa 21 ,kilometa tano pamoja na kilometa mbili na nusu kwa ajili ya watoto ambapo alitaja zawadi kuwa mshindi wa kwanza wa kilometa 21 atapata milioni moja ,mshindi wa pili atapata laki tano ,na mshindi wa tatu atapewa laki tatu.
Alitaja malengo ya mbio hizo ni kupiga vita ujangili pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.
"Unajua wananchi wengi na maanisha wa Tanzania wengi wamekuwa na tabia ya kutotembelea hifadhi zetu za taifa hivyo mbio hizi zitasaidia kuhamasisha wa Tanzania kuwa na tabia ya kutembelea hifadhi zetu" alisema Meta
Alisema kuwa kwa washindi wa mita zote ambao watashika kuanzia Namba tano hadi kumi wao watapata fursa ya kutembelea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro kwa ajili ya kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo.
Alitoa wito kwa wa Tanzania kujitokeza kushiriki mbio hizo .
Muandaaji wa Ngorongoro marathon akizungumza na Mwandishi wa habari hizi hii leo
Hivyo makala WANARIADHA MASHUHURI KUSHIRIKI NGORONGORO MARATHONI APRIL 20
yaani makala yote WANARIADHA MASHUHURI KUSHIRIKI NGORONGORO MARATHONI APRIL 20 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANARIADHA MASHUHURI KUSHIRIKI NGORONGORO MARATHONI APRIL 20 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/wanariadha-mashuhuri-kushiriki.html
0 Response to "WANARIADHA MASHUHURI KUSHIRIKI NGORONGORO MARATHONI APRIL 20"
Post a Comment