Loading...

WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA

Loading...
WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA
link : WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA

soma pia


WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA

 Picha ya pamoja ya washriki wa mkutano wa mafunzo kwa baadhi ya wataalam na wahandisi katika kilimo cha Umwagiliaji yaliyofanyika mapema jijini Dodoma leo.
 katika picha Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Uendeshaji na Matunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Anthon Nyarubamba akiongea na wandishi wa habari hawapo katika picha kuhusu matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji
Katika Picha Mkurugenzi wa Idara ya Ufanisi na Utafiti kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Muyenjwa Maugo akiongea na waandishi wa Habari hawapo katika picha mara bada ya mkutano wa Mafunzo kwa wahandisi na wataalam katika eneo la kilimo cha umwagiliaji jijini Dodoma leo
katika picha ni Sehemu ya washiriki wa kikao cha mafunzo cha wahandisi na wataalam katika kilimo cha umwagiliaji kilichofanyika jijini Dodoma leo.



NA; MWANDISHI MAALUM - DODOMA

Imeelezwa kuwa Serikali kwa kushirikina na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan JICA kwa kupitia mradi wa kujengea uwezo wataalam nchini katika eneo la umwagiliaji imewapatia wahandisi na wataalam katika eneo la kilimo cha umwagiliaji mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo katika eneo la Mradi.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Usanifu na Utafiti Mhandisi Muyenjwa Maugo kutoka Tume ya Taifa ya umwagiliaji, ambapo Maugo alisema sambamba na hilo mradi pia umeendelea kutoa miongozo ikiwa ni pamoja na vitendea kazi vitakavyotumika katika ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji na upembuzi yakinifu ambapo ameeleza kuwa awali hakukuwa na muongozo katika skimu za miradi ya umwagiliaji jambo ambalo lilisababisha shughuli za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kutofanyika katika ubora unaostahili.

“Serikali inatumia rasimali nyingi kama vile fedha ili kuhakikisha miundombinu ya umwagiliaji inakuwa katika ubora unaostahili hivyo hatutaweza kuvumilia uendeshaji na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji usiofuata utaratibu na hatimaye kuwa chini ya kiwango.” Alisema Maugo.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Uendeshaji na Mtunzo Bw. Anthony Nyarubamba alisema kuwa Uelelimishaji katika eneo la utunzaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagilaji unaweza kuongeza tija katika eneo la uzalishaji wa chakula katika skimu nyingi za umwagiliaji nchini kwani muitikio kwa wakulima ni mkubwa mno. Akitolea mfano wa skimu ya kilimo cha umwagiliaji cha Igomelo Mkoani Mbeya ,Bw. Nyarubamba amasema kabla ya bei ya kitunguu kuharibika mkulima wa zao hilo alikuwa akipata takribani shilingi miloni Arobaini (40) kwa mwaka.

Aidha Bw. Nyarubamba amesema ili Nchi iweze kuingia vizuri katika uchumi wa Viwanda kilimo cha umwagiliaji kikitumika vizuri Nchi inaweza kupata malighafi za viwanda na kujipanga kulingana na masoko kutokana na upatikanaji wa mazao ya kutosha.


Hivyo makala WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA

yaani makala yote WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/wataalam-kilimo-cha-umwagiliaji-nchini.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WATAALAM KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPIGWA MSASA"

Post a Comment

Loading...