Loading...
title : WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA - DKT. GEORDAVIE KASAMBALE
link : WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA - DKT. GEORDAVIE KASAMBALE
WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA - DKT. GEORDAVIE KASAMBALE
Na Woinde Shizza wa Michuzi TV, Arusha
Watanzania dumisheni amani na upendo uliopo katika nchi yetu kwani ndio zawadi pekee tulioachiwa na mwenyezi Mungu, amesema Nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako Dkt. Geordavie Kasambale (pichani) jijini hapa wakati akiongea na waumini Wa kanisa hilo katika ibada ya Chuo cha Manabii kilichopo Kisongo.

Alisema kuwa Watanzania tunayo amani ambayo tumezawadiwa na Mungu hivyo ni wajibu wa kila MTU kuienzi, kuidumisha pamoja na kuilinda.
"Unajua Mungu anatupendelea sana Watanzania. Ametupa amani ya nchi yetu...ametufanya tunaishi kwa upendo. Hebu angalieni nchi zingine wanapigana kila siku... Kuna vita ndugu kwa ndugu hawapendani. Lakini sisi Watanzania tunaishi kwa amani hivyo ni vyema amani hii tuliopewa tuilinde kama vile mboni ya jicho letu" alisema Geordavie
Aidha aliwataka Watanzania kutoruhusu mtu yeyote yule kuingilia amani yetu na kuivuruga kwani hii ni zawadi ya pekee tuliopewa na mwenyenzi Mungu. Pia alimtaka kila Mwananchi kupitia imani yake kuendelea kuombea nchi yetu ya Tanzania iendelee kuwa na amani, na pia aliwakumbusha kuwaweka viongozi wetu wa kitaifa akiwepo Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania katika maombi kila siku ili mungu aendelee kuwaongoza na kuwapigania.
Dkt. Kasambale amewataka Watanzania kutii Sheria za nchi bila vurugu, huku akisisitiza wanasiasa kutopandikiza chuki miongoni mwa wananchi badala yake wawaunganishe na kuwafanya kitu kimoja.
Hivyo makala WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA - DKT. GEORDAVIE KASAMBALE
yaani makala yote WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA - DKT. GEORDAVIE KASAMBALE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA - DKT. GEORDAVIE KASAMBALE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/watanzania-dumisheni-amani.html
0 Response to "WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA - DKT. GEORDAVIE KASAMBALE"
Post a Comment