Loading...

WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI

Loading...
WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI
link : WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI

soma pia


WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI

Na Emmanuel Madafa, Mbeya
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, SSP James Kasusura,amewasimamisha kazi watendaji wa Kata 11 kwa tuhuma za kutafuna fedha za Milioni 73 za vitambulisho vya biashara kwa wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi huyo amesema, March 29, 2019 ofisi hiyo iliendesha zoezi la uhakiki wa vitambulisho hivyo na kubaini kiasi cha shilingi milioni 73 kilikuwa hakijaingizwa kwenye akaunti ya halmashauri.

Amefafanua kuwa hali hiyo iliwasababishia kwenda kufanya uhakiki wa vitambulisho hivyo kwa wahusika na kubaini kwamba kiasi cha shilingi milioni 19 kilikuwa kimetafunwa na watumishi hao ambao si waadilifu.

“Utaratibu wa fedha za vitambulisho umeweka wazi kwamba vitambulisho vinapouzwa basi fedha za malipo yote yanaingizwa kwenye akaunti ya malipo ya halmashauri jambo ambalo watumishi hawa  hawakulitekeleza.”Amesema Kasusura.

Mkurugenzi huyo aliwataja watumishi hao kuwa ni  Clever Mamakula anadaiwa shilingi 700,000, Anjelo Mbinda shilingi milioni 1.5, Ayubu Thomos Mweikaja shilingi 980,000, Tito Mwasyoki anadaiwa shilingi 600,000, Elmani Kapinga shilingi 800,000 na Baraka Mwabuponda shiingi milioni 1.4.
Hata hivyo, alisema watumishi wote wameandikiwa barua ya kusimamishwa kazi na wamekabidhiwa polisi na kwamba aratibu za kisheria zitafuatwa kwani bado wengine wanachunguzwa.

Aidha, amesema watumishi hao wamefikishwa mikononi mwa polisi kwa ajili ya uchunguzi na endapo watabainika kukiuka agizo, sheria na taratibu za usambazaji wa vitambulisho hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Hivyo makala WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI

yaani makala yote WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/watumishi-11-wasimamishwa-kazi-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATUMISHI 11 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTAFUNA FEDHA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI"

Post a Comment

Loading...