Loading...

WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA

Loading...
WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA
link : WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA

soma pia


WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aakizungumza na wananchi wa Kata ya Ilolangulu Wilayani Mbogwe, Mkoani Geita (hawapo pichani) baada ya kusikiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Ilolangulu Wilayani Mbogwe wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani) alipokuwa anazungumza nao baada ya kusikiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoani Geita, baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Ilolangulu wilayani humo, akiskiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani na Nchi


Na Mwandishi Wetu, Geita.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbogwe (OC CID) Mkoani Geita, pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa kuomba na kupokea rushwa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata za Ilolangulu na Busabaga wilayani humo, Lugola alisema Polisi hao ambao waliomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni nne kutoka kwa wananchi wa Kata hizo

ambao walikuwa wanataka kuwaombea dhamana ndugu zao, ndipo polisi hao wakaomba fedha kiasi hicho ili watolewe mahabusu ya Polisi katika Kituo cha Polisi Mbogwe.Maafisa hao wa Polisi ambao wanadaiwa kupokea rushwa kutoka kwa wananchi hao ni OC CID wa Wilaya hiyo, Luitiko Kibanda na Mkaguzi wa Polisi aitwaye kwa jina la Kessy ambao wananchi hao pamoja na Mbunge wao
walisema waliwakabidhi fedha kiasi hicho.

”Wananchi walipitisha mchango kila kaya ili kuwanusuru wenzao na viongozi wao haikutosha wakamuomba Mbunge wao akawachangia shilingi laki tano pia wakachukua na hela yao iliyokuwa ni ya kujengea zahanati wakawapelekea polisi, bila hata aibu polisi hawa wakachukua fedha hizo, bila kujali hali za kiuchumi walizonazo wananchi hao”alisema Lugola.

Lugola alisema licha ya Kata hizo kukithiri vitendo vya wizi na ubakaji na Polisi kufanya wajibu wao kuwakamata watuhumiwa mbalimbali, lakini ni kosa kuwaonea wananchi kwa kuwaomba rushwa kupitia kisingizio cha utoaji wa dhamana huku sheria ikieleza kwa makosa yanayodhaminika dhamana itolewe kwa mujibu wa sheria na siyo kuwanyanyasa wananchi.

Aidha, Waziri Lugola alitoa onyo kwa Polisi nchini ambao wanawafanya wananchi mtaji kwa kuwabambikiza kesi kisha kuwaomba pesa, kuacha tabia hiyo mara moja na endapo wakibainika hatawavumilia, hatawaonea huruma
hivyo sheria itafuata mkondo wake.

Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Ikobe, Wilayani humo, Costantine Kwezi, alimuomba Waziri kuwasaidia kukamilisha kituo cha polisi katika Kata yake na pia kuongeza idadi ya askari kituoni hapo, kwasababu kituo hicho kina askari mmoja ambaye anazidiwa na majukumu.

Baadhi ya kina mama katika mkutano huo, nao walimuomba Waziri huyo kuwasaidia waume zao waliokamatwa kwa kosa la kusingiziwa kuwa ni majambazi kuachiwa huru, kutokana na kukosa hela ya kuhudumia familia na wao wameachwa bila kazi na watoto wadogo.


Hivyo makala WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA

yaani makala yote WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/waziri-lugola-amsimamisha-kazi-mkuu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA"

Post a Comment

Loading...