Loading...

WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI

Loading...
WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI
link : WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI

soma pia


WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempongeza mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF) kwa kazi kubwa iliyofanywa na Shirika hilo hapa nchini. Ametoa pongezi hizo leo (Alhamisi, Aprili 11, 2019) alipokutana na mwakilishi wa UNICEF, Bibi Maniza Zaman ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amempongeza Bibi Zaman kwa upendo mkubwa aliouonesha kwa watoto wa Tanzania hasa katika kusimamia masuala ya afya, elimu na haki za watoto wa kike. “Tumenufaika na mengi kutoka UNICEF wakati ukiwa hapa hasa kwenye masuala ya haki za watoto,” amesema na kuongeza:

“Utendaji wako wa kazi katika nyanja hizi uliwezesha tufanye kazi kwa utulivu kwa sababu ulikuwa ukisukuma mambo mengi, kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini. Tunasikitika kwamba utaondoka hivi karibuni lakini tunakutakia heri na maisha mema huko uendako Kenya.”

Kwa upande wake, Bibi Zaman ambaye amekaa hapa nchini kwa miaka mitatu na miezi minne, amesema anaishukuru Serikali kwa ushirikiano iliompatia kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini. “Ninaona siku zimeisha haraka sana, lakini ninashukuru viongozi mbalimbali kwa ushirikiano walionipatia,” amesema.

Amesema katika kipindi chote hicho, ameshirikiana vizuri na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, na wizara nyingine tano za kisekta ambazo amekuwa akifanya nazo kazi kwenye masuala ya watoto. Bibi Zaman amesema jambo kubwa la kujivunia ni mafanikio yaliyopatikana kwenye kazi ya kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri usiozidi miaka mitano ambayo ilifanyika kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).

“Tuliweza kuunda mfumo rahisi wa kusajili watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambao iliwasaidia kupata vyeti ndani ya siku moja na tumeweza kuifikia mikoa 13 ambayo ni nusu ya mikoa yote hapa nchini. Kazi hii imewezesha watoto milioni 3.5 wapate vyeti vya kuzaliwa na kuongeza kiwango cha watoto wenye vyeti hivyo, iongezeke kutoka asilimia 13 hadi kufikia asilimia 38 katika kipindi cha miaka minne na nusu,” amesema.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Mwanza, Lindi na Geita. Mingine ni Shinyanga, Mara, Simiyu, Mtwara, Dodoma na Singida. Amesema ana imani kuwa kwa mikoa iliyobakia, kazi hiyo itakamilika pindi fedha zitakapopatikana. Pia amepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupunguza tatizo la utapiamlo. Maeneo mengine ambayo wamefanyia kazi ni elimu na afya.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Maniza Sultan Zaman, walipokutana kwa mazungumzo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Maniza Sultan Zaman, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa picha ya watoto na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Maniza Sultan Zaman, baada ya mazungumzo yao, ofisini Magogoni, jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Hivyo makala WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI

yaani makala yote WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/waziri-mkuu-ampongeza-mwakilishi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU AMPONGEZA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI"

Post a Comment

Loading...