Loading...
title : CCM Z’BAR YATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MSHAURI WA MASUALA YA UTENZI ,IDARA YA UENEZI.
link : CCM Z’BAR YATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MSHAURI WA MASUALA YA UTENZI ,IDARA YA UENEZI.
CCM Z’BAR YATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MSHAURI WA MASUALA YA UTENZI ,IDARA YA UENEZI.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdalla Juma Saadalla “Mabodi” , kwa niaba ya wafanyakazi na wanachama wote wa CCM amewatumia salamu za rambi rambi wanafamilia, wa Marehemu Bi. Rahma Rashid kilichotokea April 17 mwaka huu, nyumbani kwake Magomeni Unguja.
Dkt. Mabodi alisema Chama kimepokea kwa masikitiko ,majonzi na huzuni mkubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa mwanachama wake huyo , ambaye wakati wa uhai wake alijitolea muhanga kwa maslahi ya CCM.
Alitoa pole kwa familia ya Marehemu na kuongeza kuwa Chama hicho kinaungana na ndugu, marafiki na watu wa karibu wa
na kuongeza kuwa Chama kinatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya msiba huo.
Marehemu huyo, ambaye enzi za uhai wake alikuwa ni mshauri wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar katika masuala ya Sanaa ya utenzi, kazi aliyofanya kwa ufanisi mkubwa.
Alieleza kwamba enzi za uhai wake Marehemu huyo alikuwa ni miongoni mwa Watunzi mashuhuri wa Tenzi mbali mbali zikiwemo za kielimu, kijamii na kisiasa ambazo zilimpatia sifa ndani na nje ya Zanzibar.
“Marehemu Bi.Rahma ataendelea kubaki katika kumbukumbu za Chama chetu kutokana na uhodari wake katika masuala mbali mbali ya kijamii na kisiasa hasa kwa mambo yaliyokuwa yakihusu chama chetu.
Wakati wote alikuwa tayari kufanya kazi za Chama bila ya kujali muda wala maslahi ya binafsi, hivyo na sisi tuliobaki tukiwa hai kwanza tufuate nyayo zake kwa kuwa waadilifu na wazalendo kwa Nchi na Chama pia tumuuombee Dua yeye pamoja na Wazee wetu waliotangulia mbele ya haki uko walipo wapumzike kwa amani.”, alisisitiza Dkt. Mabodi na kuongeza kuwa CCM itaenzi mambo mema aliyayaacha kwa vitendo.
Wasifu wa Marehemu huyo ambaye alikuwa ni Mwalimu wa Skuli za msingi hapa Unguja na baadae kuteuliwa kuwa Mnukuu wa Ikulu Zanzibar na kufanya kazi hapo hadi lustaafu kwake na amefariki akiwa nab umri wa miaka 69.
Tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Bi.Rahma Rashid , Mahala pema peponi . Amin.
Hivyo makala CCM Z’BAR YATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MSHAURI WA MASUALA YA UTENZI ,IDARA YA UENEZI.
yaani makala yote CCM Z’BAR YATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MSHAURI WA MASUALA YA UTENZI ,IDARA YA UENEZI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM Z’BAR YATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MSHAURI WA MASUALA YA UTENZI ,IDARA YA UENEZI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/ccm-zbar-yatoa-salamu-za-rambi-rambi.html
0 Response to "CCM Z’BAR YATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MSHAURI WA MASUALA YA UTENZI ,IDARA YA UENEZI."
Post a Comment