Loading...
title : SERIKALI YACHUKUA HATUA MBADALA KUENDANA NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA.
link : SERIKALI YACHUKUA HATUA MBADALA KUENDANA NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA.
SERIKALI YACHUKUA HATUA MBADALA KUENDANA NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA.
Na Daudi Manongi
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imechukua hatua mahsusi katika kukabiliana na changamoto zitokanano na Agenda ya Mabadiliko ya Umoja wa Ulaya.
Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha tisa na mkutano wa Saba wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Suzan Kolimba wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge Mjini Dodoma.
“Umoja wa Ulaya ivi sasa unatekeleza Agenda ya Mabadiliko ikiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa Sera ya Maendeleo ya Umoja huo,Mabadiliko haya yanahusisha kanuni mbalimbali za kutoa misaada ya Maendeleo,na mkakati huo umeainisha maeneo yaliyopewa kipaumbele ikiwemo Masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Usawa wa Kijinsia,Vyama vya Kiraia na Serikali za Mitaa,Rushwa,Sera na Usimamizi wa Kodi na Usimamizi wa Sekta ya Umma”,Alisema Mhe.Kolimba.
Amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali ambazo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kusimamia matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha tunapunguza utegemezi kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Pia Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia Sera ya Ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi ya mwaka 2009 na sheria ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi ya mwaka 2010, ambapo mkakati huu unasaidia kuongeza wigo wa vyanzo za fedha za kugharamia miradi ya maendeleo na kupunguza utegemezi kwa wahisani.
Hata hivyo Serikali inaendelea kuwashawishi wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza zaidi nchini na zinaenda sambamba na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara nchini na kupunguza gharama za kufanya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi kuwekeza nchini.
Katika kuratibu uhamasishaji wa watanzania waishio ughaibuni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeanzisha Idara maalum ya kuratibu masuala ya Diaspora ili kushiriki katika Maendeleo ya Nchi ikiwemo kuwekeza nchini.
Hivyo makala SERIKALI YACHUKUA HATUA MBADALA KUENDANA NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA.
yaani makala yote SERIKALI YACHUKUA HATUA MBADALA KUENDANA NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YACHUKUA HATUA MBADALA KUENDANA NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/serikali-yachukua-hatua-mbadala.html
0 Response to "SERIKALI YACHUKUA HATUA MBADALA KUENDANA NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA."
Post a Comment