Loading...
title : HALMASHAURI YA ARUSHA YAJIKITA KATIKA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA
link : HALMASHAURI YA ARUSHA YAJIKITA KATIKA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA
HALMASHAURI YA ARUSHA YAJIKITA KATIKA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA
Watumishi wa Idara ya maendeleo ya Jamii halmashauri ya Arusha wanaendelea kutekeleza majukumu yao kwa kutoka ofisini na kwenda kwenye jamii kutoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya pombe haramu ya gongo.
Afisa maendeleo ya jamii Bi Getrude Darema (mwenye kupata sauti) akiongea na wanajamii katika soko la Oldonyosambu kuhusu madhara ya madawa ya kulevya |
Afisa Maendeleo ya Jamii ndugu Getrude Darema ameiongoza timu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya wilaya kwa kushirikiana na watumishi wa kata za Olkokola na Oldonyowasi kuwaelimisha wananchi wa rika zote kwa makundi kwenye soko la Oldonyosambu na kutoa elimu ya kuachana na kilimo, biashara pamoja na matumizi ya bangi na pombe haramu ya gongo.
Bi Getrude amewataka vijana waliokuwa katika soko la Oldonyosambu kuchana kabisa na matumizi ya bangi na pombe haramu ya gongo kwani ni kinyume cha sheria na zaidi inawaathiri vijana hao kiafya na kuwa na vijana wasio na uwezo wa kufanya kazi kabisa. Pia aliendelea kuwasisitiza vijana kuachana na kupiga vita ndoa za utotoni na ukeketaji wa watoto wa kike kwani vijana ndio nguzo ya mabadiliko katika jamii yao.
Bi Getrude amewasihi wazazi kuwa licha ya changamoto nyingi za maisha lakini wanatakiwa kutenga muda wa kukaa na watoto wao kuwasikiliza na kuwaelemisha juu ya madhara ya dawa za kulevya, matumizi ya pombe haramu ya gongo na kuwasisistiza watoto wao kuzingatia masomo na umuhimu wa elimu katika maisha yao.
"Kutokana na hali ya maisha ya sasa kila mtu anahangaika kufanya kazi akitoka asubuhi anarudi usiku hana muda wa kukaa na watoti, lakani mkumbuke kuwa malezi ya watoto ni jukumu la wazazi hivyo pangeni muda wa kukaa na watoto wenu ili msikilize matatizo yao"alisema Getrude.
Aidha amewaisitiza wakazi hao kukataa na kupinga unyanyasaji wa watoto kwa kuwafichua watu wanaowadhalilisha watoto kwa kuwabaka, kuwaona na kuwapa mimba wakiwa bado shuleni.
Mkazi wa kijiji cha Lemong'o, Bi Nganashe Losieku amewashukuru watumishi wa halmashauri kwa elimu waliyoitoa kwa kuwa jamii yao inakabiliwa na changamoto zote zilizoainishwa za biashara na matumizi ya bamgi, ukeketaji pamoja na ndoa za utotoni kutokana na mila na desturi zao.
"Hii elimu ni muhimu sana inasaidi watu kukabiliana na matatizo mengi yanayotukabili kutokana na mila na desturi za kabila letu la kimaasai ingawa kwa sasa watu wameanza kubadilika taratibu na nyinyi msichoke kuja mara kwa mara kukumbusha watu wa huku" alisema Nganashe.
Pichani ni makundi ya rika tofauti yalipewa elimu kwenye soko la Oldonyosambu
Hivyo makala HALMASHAURI YA ARUSHA YAJIKITA KATIKA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA
yaani makala yote HALMASHAURI YA ARUSHA YAJIKITA KATIKA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALMASHAURI YA ARUSHA YAJIKITA KATIKA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/halmashauri-ya-arusha-yajikita-katika.html
0 Response to "HALMASHAURI YA ARUSHA YAJIKITA KATIKA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA"
Post a Comment