Loading...
title : IRAN YAONESHA NIA KUWEKEZA NCHINI
link : IRAN YAONESHA NIA KUWEKEZA NCHINI
IRAN YAONESHA NIA KUWEKEZA NCHINI
Na Veronica Simba – Dodoma
Balozi mpya wa Iran hapa nchini, Mousa Farhang amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumzia uwezekano wa nchi za Tanzania na Iran kushirikiana katika sekta za nishati na madini.
Balozi Farhang alimtembelea Profesa Muhongo jana, Aprili 28, 2017 ofisini kwake mjini Dodoma.
Akizungumzia nia ya nchi yake kushirikiana na Tanzania katika sekta ya nishati, Balozi Farhang alimwambia Waziri Muhongo kuwa Iran inazo sifa stahiki katika sekta hiyo kutokana na maendeleo iliyofikia ambapo alieleza kuwa mbali na kuzalisha umeme wa kutosha kwa mahitaji ya nchi, imejenga viwanda vya umeme katika baadhi ya nchi zinazowazunguka.
Aidha, aliongeza kuwa, nchi hiyo huzalisha zaidi ya mapipa milioni nne ya mafuta kwa siku moja.
“Miaka 10 iliyopita, Iran ilikuwa kama nchi nyingine zilizo nyuma kimaendeleo lakini sasa tunazalisha umeme mwingi unaotosheleza mahitaji ya nchi yetu na mwingine tunauza.
Alisema kuwa, kutokana na utafiti alioufanya yeye binafsi, amegundua kuwa, sekta ya nishati ndiyo yenye nafasi kubwa na nzuri zaidi itakayowezesha nchi za Tanzania na Iran kunufaika endapo zitashirikiana.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akifafanua jambo kwa Balozi mpya wa Iran hapa nchini, Mousa Farhang (katikati), wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri ofisini kwake mjini Dodoma hivi karibuni. Kulia ni Ofisa kutoka Ubalozini, Maisarah Ally.
Balozi mpya wa Iran nchini Tanzania, Mousa Farhang (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Balozi Farhang alimtembelea Waziri Muhongo ofisini kwake mjini Dodoma hivi karibuni.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiagana na Balozi mpya wa Iran nchini Tanzania, Mousa Farhang (kulia). Katikati ni Ofisa kutoka Ubalozini, Maisarah Ally.
Hivyo makala IRAN YAONESHA NIA KUWEKEZA NCHINI
yaani makala yote IRAN YAONESHA NIA KUWEKEZA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala IRAN YAONESHA NIA KUWEKEZA NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/iran-yaonesha-nia-kuwekeza-nchini.html
0 Response to "IRAN YAONESHA NIA KUWEKEZA NCHINI"
Post a Comment