Loading...

KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI

Loading...
KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI
link : KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI

soma pia


KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI

mwambawahabari
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo (Kushoto) akionyeshwa na Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG toka nchini India maeneo ambayo maji yanapita kuelekea kwa wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi katika eneo la tanki la maji safi lililopo Kibamba 19 Aprili, 2017.

Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (DAWASA), Bw. Romanus Mwangingo (aliyevaa tai) akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo kuhusu maendeleo waliyofanya katika kusambaza maji kwa wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi katika eneo la tanki lililopo Kibamba 19 Aprili, 2017.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG, Watendaji toka DAWASA na DAWASCO wakati wa ziara yake ya kikazi leo 19 Aprili, 2017.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akimsikiliza Meneja wa Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) Kibaha, Bw. Erasto Mbwambo wakati akieleza taarifa ya maendeleo ya usambazaji maji kwa wananchi wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo leo 19 Aprili, 2017.

Baadhi ya Maofisa Waandamizi wa DAWASA na DAWASCO wakifuatilia taarifa ikiyosomwa na Meneja wa Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) Kibaha, Bw. Erasto Mbwambo (hayupo pichani) mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo leo 19 Aprili, 2017.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo(wa pili kushoto) akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali na Watendaji wa DAWASA na DAWASCO pamoja na Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG ya nchini India wakielekea katika sehemu ya mtambo wa kusukuma maji (IN TAKE) ambao unasukuma maji kwenda mtambo wa Ruvu Juu 19 Aprili, 2017.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG ya nchini India wakati alipofika eneo la Mto Ruvu kujionea namna maji yanavyokusanywa na kusukumwa kwenda mtambo wa Ruvu Juu 19 Aprili, 2017.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo pamoja na Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG ya nchini India wakiwa katika mazungumzo katika eneo la mtambo wa Ruvu Juu 19 Aprili, 2017.



Na Mwandishi Wetu.


KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiaji Prof. Kitila Mkumbo leo ametembelea Mtambo wa Ruvu Juu uliopo eneo la Mlandizi Mkoani Pwani na kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali kupitia Wizara anayoiongoza.
    

Akiwa mtamboni hapo alipata fursa ya kushuhudia mtambo huo ukifanya kazi kama ilivyotarajiwa baada ya upanuzi wake kukamilika, ambapo hivi sasa mtambo una uwezo wa kuzalisha maji safi na salama kiasi cha lita milioni 196 kwa siku.  


Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani hapo, Prof. Kitila amesema kwamba ziara hiyo ni muhimu kwake kwa kuwa amejifunza mambo mengi kuhusu namna maji yanavyopatikana ambapo ametoa pongezi kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika eneo hilo.


“Uwekezaji huu ni mkubwa sana uliofanyika katika eneo hili, uwekezaji huu unahitaji kutunzawa ili kudhibti upotevu wa maji”, alisema Prof. Mkumbo.


Amewataka Mameneja wa Miradi ya Maji kuhakikisha kuwa wanajiwekea malengo katika kuwahudumia wananchi na ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha kwamba wanayatunza maji wayapatayo kwakuwa upatikanaji wake ni mrefu na Serikali imewekeza fedha nyingi katika kuyapata maji hayo.


Aidha, Serikali imetekeleza mradi huo kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) ambapo katika ziara yake hiyo ameweza kupita na kujionea maeneo mbalimbali yanayozalisha maji na kuyahifadhi ikiwemo Matenki ya maji yaliyopo eneo la Chuo Kikuu cha Ardhi yenye ujazo wa lita milioni 45, tenki la maji safi la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni 10, Ruvu Darajani (In-take), Mtambo mpya wa Ruvu Juu.


Sambamba na ziara hiyo, Prof. Kitila alipata wasaa wa kutembelea Ofisi ya Dawasco iliyopo Kibaha na kuktana na watendaji wa ofisi hiyo akiwemo Meneja wa DAWASCO Kibaha, Bw. Erasto Mbwambo ambaye alitoa taarifa yake kuhusu maendeleo yaliyofikiwa katika kuhakikisha kuwa maji yanawafikia wananchi jambo ambalo lilimfurahisha Prof. Kitila.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Bw. Romanus Mwangingo ameeleza kuwa, kwa sasa tayari maji toka Mtambo wa Ruvu Juu yameanza kuzalishwa baada ya shughuli za upanuzi katika mtambo huo kakamilika.


Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na kuhudhuriwa na Maofisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, DAWASA, DAWASCO, Wakandarasi pamoja na Mshauri wa mradi wa mfumo wa maji wa Ruvu Juu.


Hivyo makala KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI

yaani makala yote KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/katibu-mkuu-wizara-ya-maji-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI"

Post a Comment

Loading...