Loading...

KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA

Loading...
KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA
link : KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA

soma pia


KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA

Uliwahi kupata email kutoka kwa mtu anayejiita Prince wa huko Nigeria akikutaka uconfirm taarifa za bank akutumie fedha kwa ajili ya kuanzisha kampuni au kufanya nae biashara kama mbia na ukapuuzia? basi ungana na watu wengi kujutia


Sasa hili limekuwa ni mada mitandaoni watu wakifanya utani wakijutia kutokujibu email ya "prince" baada ya kikosi cha kupambana na rushwa Nigeria (EFCC) kufanikiwa kukamata fedha taslimu kiasi cha dola million 43 za kimarekani katika nyumba tupu ya kupanga huko jijini Lagos.


Taarifa rasmi ya EFCC inasema kuwa walifanikiwa kuokoa fedha hizo katika Jumba (appartment) lisilokuwa na watu baada ya mtu (whistleblower) kuwapa taarifa kuwa kuna wanawake wenye nguo chafuchafu wanabeba mabegi kuingiza na kutoa katika nyumba hiyo. Taarifa hiyo inasema kuwa walifanikiwa pia kupata Naira (Nigerian currency) milion 23.2 sawa na dola elfu 75, na pound 27,800 sawa na dola elfu 35 zikiwa zimepangwa vizuri ndani ya kabati la mbao lililofichwa katika chumba cha kulala.


Taasisi hiyo ya kupambana na rushwa imesema mpaka sasa hakuna aliyekamatwa kuhusika na fedha hizo na inawezekana zilikuwa za magendo kwa ajili ya matukio yasiyo ya kisheria.
Mapema wiki hii Taasisi hii ya kupambana na rushwa ilisema walifanikiwa kupata dola 817,000 katika soko moja huko Lagos na nyingine dola 1.5 million katika duka moja huko huko Lagos. 

Waziri wa fedha wa Nigeria amepongeza sera mpya ya kutoa taarifa (whistleblowing policies) iliyoanza mwezi Desemba 2016. Watoa taarifa wamewezeshwa kutumia mfumo wa siri wa kutoa taarifa na kama taarifa zao zitafanikiwa kupatikana kwa fedha za umma zilizochakatishwa, huyo mtoa taarifa atapata kati ya 2.5% hadi 5% ya fedha zote zilizokamatwa. 

Mwezi Februari, Waziri wa habari, ndugu Lai Muhamed alisema sera hii mpya imefanikisha kukamatwa kwa zaidi ya dola billion 180.


Source: CNN



Hivyo makala KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA

yaani makala yote KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/kikosi-cha-kupambana-na-rushwa-nigeria.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KIKOSI CHA KUPAMBANA NA RUSHWA NIGERIA IMEKAMATA DOLA MILLION 43 KWENYE NYUMBA YA KUPANGA"

Post a Comment

Loading...