Loading...

Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha

Loading...
Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha
link : Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha

soma pia


Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha



Mch.Dr.Jerry Williamson kutoka nchi Marekani akiomba katika ibada ya katika kongamano kanisa la Zion lililopo njiro jijini Arusha ambapo kanisa hilo limeendaa semina na kongamano kwa wachungaji pamoja na washirika wengine,kulia kwake ni Ben Mangeni ambaye ni mkalimani wake



Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo akiongea na waandishi wa habari , alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki kongamano hilo wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine

Mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.

kushoto ni Mtume trice Shumbusho akiwa na mkalimani wake akihubiri katika kongamano hilo

Waumini wakiwa katika maombi

Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano

Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano

Picha ikionyesha madhabahuni

Picha ikionyesha jengo la kanisa

Na Pamela Mollel,Arusha

Wachungaji zaidi ya 300 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila kujali madhehebu yao wako katika semina maalumu ya neno la Mungu yenye lengo la kusaidia kupeleka ujumbe wa madhihilisho ya nguvu ya kristo katika maeneo mbalimbali ya nchi ili watu waweze kubadilika na kumjua Mungu


Semina hiyo ya siku nane iliyoandaliwa na kanisa la Zion City Church Arusha litafanyika kanisani hapo ikiambatana na Kongamano ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wachungaji na watu mbalimbali likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleka injili kwa watu wa mataifa.


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine.


Mngodo aliongeza kuwa huduma zitakazo tolewa katika katika kongamano hilo hazitawakugusa kiroho tu bali hata kwenye maisha yao ya kawaida wataweza kubadilika

“Tunaamini kongamnao hili litagusa wachungaji hawa na jamii wanayoihudumia kimwili na kiroho”alisema Mngodo


Kwa upande wake mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.

Mch.Sule alisema kuwa ulimwengu wa sasa umeharibika hivyo unahitaji watumishi waliokutana na Mungu na si wanaomjua Mungu pekee ili waweze kuwatumikia watu.

Miongoni mwa watumishi wa Mungu wa kimataifa watakao kuwa wasemaji wakuu katika kongamano hilo ni Askofu mkuu wa kanisa la Zion City Church Arusha John Shumbusho pamoja na mkewe Trice Shumbusho


Wachungaji wengine ni kutoka nje ya nchi Mch.Dr.Jerry Williamson, Mch.Dr Jim Oxendine kutoka Marekani,Mch.Yoshua Masasu kutoka Rwanda,Mch.Aloysius Kiiza kutoka Uganda,Pamoja na Mch.George Mkandawire kutoka Afrika Kusini .


Hivyo makala Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha

yaani makala yote Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/matukio-kongamano-la-wachungaji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matukio : Kongamano la Wachungaji kufanyika Jijini Arusha"

Post a Comment

Loading...