Loading...

Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo

Loading...
Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo
link : Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo

soma pia


Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO - DODOMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.


Akizungumza, leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.


“Tunapoadhimisha miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama


Pia, Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya maadhimisho hayo.


“Wananchi wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema Rugimbana


Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.


Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.


Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.



Waziri Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri leo Mjini Dodoma.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia maonesho ya maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu Serikali ilipohamia Dodoma.

Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.



Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.



Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.

Askari wa Pikikipi maalum wakionesha namna pikipiki hizo zitakavyopamba maonesho hayo.

Makomandoo wa Jeshi la wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari lenye tani 7 ikiwa ni moja ya mbinu ya medani katika uwanja wa mapambano.

Askari wa Kikosi cha Farasi wakionesha umahiri wao katika kutumia farasi kupambana na uhalifu.



Wanafunzi wa halaiki wakipita kwa ukakamavu mbele ya Jukwaa Kuu


Hivyo makala Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo

yaani makala yote Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/matukio-watanzania-waaswa-kuwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matukio : Watanzania Waaswa kuwa Wazalendo na Kulinda Amani Iliyopo"

Post a Comment

Loading...