Loading...
title : MKANDARASI AANZA KAZI USAMBAZAJI MAJI PEMBEZONI MWA BOMBA KUU RUVU JUU.
link : MKANDARASI AANZA KAZI USAMBAZAJI MAJI PEMBEZONI MWA BOMBA KUU RUVU JUU.
MKANDARASI AANZA KAZI USAMBAZAJI MAJI PEMBEZONI MWA BOMBA KUU RUVU JUU.
Na Daudi Manongi
mwambawahabari
Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa mkandarasi ameanza kazi ya ujenzi wa mabomba ya usambazaji katika maeneo ya Malamba Mawili,Msigani,Mbezi Luisi,Msakuzi,Kibamba,, Kiluvya,Mloganzila na Mailimoja na atakamilisha kazi hiyo mwaka huu 2017.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe wakati akijibu hoja mbalimbalia za wabunge.
“Baada ya kukamilika kwa mradi maeneo mengi ndani ya kilomita 12 ya pembezoni mwa bomba kuu la Ruvu Juu yameanza kupata huduma ya Maji”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
Amesema kuwa maeneo ambayo yanapata maji kwa sasa kutoka Bomba la Ruvu Juu ni pamoja na Mlandizi na vitongoji vyake, Visiga, Misugusugu, Soga, Korogwe, Picha ya Ndege, Kwa Matiasi,Tumbi, Mailimoja, Pangani, Kiluvya, Kibamba, Mloganzila, Mbezi kwa Yusufu,Mbezi Mwisho, Kimara, Mavurunza, Baruti, Kibo, Kibangu,Tabata, Segerea, Kinyerezi na Karakata.
Aidha maeneo ambayo bado hayajaanza kupata huduma ya maji yatapata huduma hiyo baada ya utekelezaji wa miradi mipya ya kujenga mtambo wa mabomba ya kusambaza maji katika maeneo yote ambayo hayana huduma hiyo, Amesema kuwa miradi hii itatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha .
Hivyo makala MKANDARASI AANZA KAZI USAMBAZAJI MAJI PEMBEZONI MWA BOMBA KUU RUVU JUU.
yaani makala yote MKANDARASI AANZA KAZI USAMBAZAJI MAJI PEMBEZONI MWA BOMBA KUU RUVU JUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKANDARASI AANZA KAZI USAMBAZAJI MAJI PEMBEZONI MWA BOMBA KUU RUVU JUU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/mkandarasi-aanza-kazi-usambazaji-maji.html
0 Response to "MKANDARASI AANZA KAZI USAMBAZAJI MAJI PEMBEZONI MWA BOMBA KUU RUVU JUU."
Post a Comment