Loading...

MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO

Loading...
MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO
link : MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO

soma pia


MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO


Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Pwani SACP Onesmo Lyanga




Na Mwamvua Mwinyi


JESHI la polisi mkoani Pwani, linamshikilia Amiri Alalae (26) mkazi wa Toptop, wilaya ya Bagamoyo kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu 30 raia wa nchini Ethiopia. 


Kamanda wa polisi mkoani humo, Onesmo Lyanga, alisema tukio hilo limetokea april 13 majira ya saa kumi usiku huko maeneo ya Kilomo kata ya Kilomo tarafa ya Yombo. 


Alieleza kuwa askari wa jeshi la polisi waliokuwa kwenye doria maeneo mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo walifanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu hao wakiwa wameingia nchini bila kibali. 

"Wakiwa wamepakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T. 824 DFG  aina ya Town hiace pickup lililokuwa likiendeshwa na Amiri Alalae "alisema kamanda Lyanga. 

Kamanda Lyanga alisema, wahamiaji waliingia nchini kwa njia ya majini wakitumia majahazi na kushukia maeneo ya bandari bubu ya Jitu Kuu kutoka nchi jirani ya Kenya. 

Alisema watawakabidhi kwa idara ya uhamiaji ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. Kamanda huyo alitoa rai kwa wananchi hasa madereva kuacha tabia ya kusafirisha wahamiaji haramu kwa lengo la kujiongezea kipato.

Alisema kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kamwe hawatakuwa na muhali na wale wote wanaofanya biashara hiyo ndani ya mkoa wa Pwani.


Hivyo makala MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO

yaani makala yote MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/msafirisha-wahamiaji-haramu-atiwa_14.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ATIWA MBARONI HUKO BAGAMOYO"

Post a Comment

Loading...