Loading...
title : Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhudumia
link : Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhudumia
Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhudumia
Mwandishi wa MAELEZO, Dodoma
Dk Hamis Kigwangalla |
SERIKALI imeanza hatua za awali za uainishaji gharama, uandaaji mfumo mbadala na upembuzi wa kina wa aina ya ubia, ili kushirikiana na sekta binafsi katika utoaji huduma za uchunguzi wa magonjwa.
Hayo yalisemwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla, wakati akijibu hoja za wabunge, Dodoma.
“Kutokana na kukua kwa kasi kwa Sayansi na Teknolojia ya Uchunguzi wa Magonjwa, Wizara inakubaliana na wazo hili juu ya kuangalia namna nzuri ya kushirikiana na sekta binafsi katika utoaji huduma hizi,” alisema Kigwangalla.
Alisema kwa kuanzia sasa, Wizara yake inafikiria kuanzisha ushirikiano kwa kupitia ukodishaji vifaa ambapo Serikali itakodisha mashine hizo ambazo zitakuwa za mbia na Serikali haitahusika na ununuzi, ufungaji na matengenezo kinga ya mashine hizo.
Alibainisha kuwa katika mfumo huo, Wizara yake itakuwa na jukumu la kusimamia utoaji huduma na itapata gawio lake kutokana na makusanyo yatokanayo na uchangiaji huduma kulingana na mkataba.
“Ni imani ya Wizara kuwa kutumia mfumo wa ubia na sekta binafsi (PPP) huduma za uchunguzi wa magonjwa zitaimarika na kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama,” alisema Kigwangalla.
Hivyo makala Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhudumia
yaani makala yote Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhudumia Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhudumia mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/serikali-kushirikiana-na-sekta-binafsi.html
0 Response to "Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhudumia"
Post a Comment