Loading...

UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI

Loading...
UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI
link : UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI

soma pia


UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI


Nteghenjwa Hosseah, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ameweka Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi Kata ya Muriet wakati wa ziara ya Kikazi Jijini hapa yenye lengo la kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi.

Akiweka jiwe la Msingi Mhe. Gambo amesema kwa muda mrefu alikua anakerwa na uhalifu uliokithiri katika eneo hilo na hali hiyo kumsukuma yeye kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa kituo cha Polisi kitakachosaidia kudhibiti masuala ya Uhalifu.

Aliongeza kuwa baada ya kumpata mfadhili huyo alimlete eneo la ujenzi ambapo pia wahalifu walimuibia Simu yake mbele ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndipo na mfadhili alipopata ari ya kuanza ujenzi huu haraka iwezekanavyo. 

“Haiwezekani mtu anaiba mbele ya Kamanda wa Polisi hakika hii ilituthibitishia kwamba uhalifu katika eneo hili umekithiri na kwa sababu hakunha Kituo cha Polisi wahalifu wanapata mwanya wa kufanya kazi hii isiyo halali kwa ujasiri zaidi” Alisema Gambo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mfadhili ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Lodhia Ndg. Haruni alisema amejitolea sehemu ya mali zake ili kuwasaidia Watanzania wenzake wanaoteseka na tabia za uhalifu zinazorudisha nyuma maendeleo 

Ujenzi wa Kituo hicho utakaogharimu zaidia ya Tsh Mil 200 utakamilika mnamo mwezi Juni 2017.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akisalimiana na waendesha boda boda, eneo la kwa kwamromboo waliohuduriia kwenye uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi
1Baadhi wa wananchi waliohudhuria kushuhudia uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi Muriet.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kushoto) akiweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Kituo cha Polisi Muriet.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kushoto) akiweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Kituo cha Polisi Muriet.
Mke wa Mfadhili Bwa.Haroun akivishwa vazi la Kimasai na wakazi wa eneo hilo kama shukrani yao kwa kujengewa Kituo cha Polisi. 



Hivyo makala UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI

yaani makala yote UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/uhalifu-kwa-mromboo-wapata-muarobaini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI"

Post a Comment

Loading...