VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI - Hallo rafiki
SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts
makala afya,
makala general,
makala kisiasa,
makala kitamaduni,
makala kiuchumi,
makala mambo mapya,
makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.
title :
VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURIlink :
VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI
VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI
Halmashauri ya wilaya ya Arusha imeendelea kutoa mikopo asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa vikundi vya kina mama na vijana.
 |
Vijana wa Umoja Youth wakiwa mbele ya duka/karakana yao
|
Kamati ya fedha, utawala na mipango ya halmashauri hiyo, wakiwa katika ziara ya miradi ya halmashauri walitembelea kikundi cha vijana kilichopo katika kata ya Moivo, kikundi cha Umoja Youth Group ambalo linaundwa na vijana 8 wenye ujuzi mbalimbali wa ufundi wa umeme na kuamua kuanzisha kikundi hicho kinachojishughulisha na ufundi wa kuchomelea (welding).
Mmoja wa vijana wa umoja youth akiwa kazini. Umoja Youth ni
miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya halmashauri
Akizungumza kwa niaba ya kikundi hicho, Ndugu Kelvin Alex Materu alisema kikundi chao kilianza mwaka 2015 na kupata usajili Agosti 2016. Kelvin alisema walianza kwa mtaji wa shilingi milion 02 tu kama mkopo wa halmashauri na kwa sasa wana mtaji wa milioni 09. Kelvin alisema wanajishughulisha na uuzaji wa nati, bolti, grili za milango, mageti na vitu vingine vya kuchomelea ambapo kwasasa wanamiliki guta ambalo hutumia kuwapelekea mizigo wateja popote walipo bure kabisa. Ili kuendelea kukuza mtaji wao, wanakikundi wamekuwa wakichangia shilingi elfu20 kila mwezi na wamekuwa wakigawana faida ya asilimia 5 kwa mwanachama kila mwezi.
 |
Kelvin Materu, kiongozi wa umoja youth akisoma risala mbele ya mwenyekiti wa halmashauri
na wajumbe wa kamati ya fedha , utawala na mipango
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Noah Lembris aliwapongeza vijana hawa na kuwaambia wawe wanaomba tenda ya kusambaza grili za milango na madirisha katika miradi ya ujenzi ya shule na zahanati zinazojengwa katika wilaya ili kuboresha mitaji yao na kuwakuza zaidi hata ikiwezekana kuanzisha kiwanda kidogo. Na amewasisitiza kuomba mkopo zaidi halmashauri ili waweza kujitanua zaidi.
 |
Mhe. Noah Lembris (wa pili kushoto), mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Arusha akiwa na wajumbe wengine wa kamati ya fedha walipotembelea mradi wa vijana wa umoja youth
|
Naye diwani wa Ilkidinga Mhe. Mungaya alisema hawa ni vijana bora wa kuigwa na wanapaswa kuwa mfano kwa kuelimisha na vijana wengine katika kata zingine ili vijana wote walioko ndani ya halmashauri ya Arusha wanufaike na mikopo hii.
 |
Bi Ahadi Mlay akitoa maelezo ya vikundi mbele ya kamati
|
Awali Afisa vijana wa halmashauri bi Ahadi Mlay alisema vijana hawa ni mfano wa kuigwa kwasababu wamekuwa wakifanya marejesho vizuri na wamepanga kuwaongezea mtaji pindi watakapomaliza mkopo huu unaotarajiwa kuisha ndani ya miezi 5. Aidha bi Ahadi alisema kwasasa kuna waraka mpya ambao mtu binafsi au saccoss inaweza kukopeshwa mpaka milion10 bila masharti magumu.
 |
Bi Ahadi afisa vijana (kushoto) akiwa na Bi Dorah ambaye ni mtendaji kata wa Moivo na mlezi wa kikundi hichi cha umoja youth
|
Kamati ya fedha ilitembelea pia miradi mbalimbali inayotekelezwa na halmashauri ya wilaya ya Arusha.
Habari katika picha
Hivyo makala VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI
yaani makala yote VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/vikundi-vya-vijana-vyanufaika-na-mikopo.html
0 Response to "VIKUNDI VYA VIJANA VYANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI"
Post a Comment