Loading...

Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini

Loading...
Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini
link : Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini

soma pia


Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini

Na Lulu Mussa, Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, hii leo amekutana na taasisi zizohusika na uratibu na usimamizi wa kemikali hapa nchini. Akiongea na Taasisi hizo, Waziri Mpina amewaagiza watendaji hao kudhibiti na kusimamia kemikali hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na kuratibu usafirishaji, usambazaji na matumizi ya kemikali hizo hapa nchini kwa namna bora zaidi.

Waziri Mpina amezitaka taasisi hizo kutoa taarifa za utendaji wa kazi kila robo ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimizi wa Mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira kifungu namba 170. “Nawaagiza kuwasilisha takwimu za kemikali zinazozalishwa nchini, zinazoagizwa au kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na kuainisha viwanda vinavyozalisha kemikali vilivyosajiliwa na maghala yaliyosajiliwa kuhifadhi kemikali hizo” alisisitiza Mpina.

Katika kikao hicho Waziri Mpina pia ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini ndani ya miezi miwili kuandaa muongozo na kuupitisha katika hatua zote wa namna bora ya kuteketeza taka hatarishi bila kuathiri mazingira.

Aidha Waziri Mpina ameagiza kuandaliwa kwa andiko litakalobainisha umuhimu wa kuteketeza taka hatarishi. “Kama taifa ni lazima tuwe na “dedicated Incinerator” kubwa kutekeza taka hizo hatarishi kwa kuzingatia taka zinazozalishwa hapa nchini” Mpina alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini, Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania, Tume ya Nguvu za Atomiki, Taasisi ya Utafiti ya Viuatilifu katika Kanda za Kitropiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa, OSHA na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa pamoja wametakiwa kuanda Hati ya Makubaliano ya kuratibu utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuhuisha Sheria zao na kuleta mapendekezo Serikali ya vifungu vya kufanyiwa marekebisho.

Taasisi alizokutana nazo ni pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC), Taasisi ya Nguvu za Atomiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Mkemia Mkuu wa Serikali.
Bw. Justine Ngaile Mkurugenzi wa Kinga na Mionzi kutoka Tume ya Atomiki akiwasilisha mada kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Luhaga Mpina. Waziri Mpini alikutana na Taasisi zinazohusika na usimamizi wa kemikali kujadilili mkakati wa pamoja wa kusimamia kemikali nchini.
Baadhi ya wataalamu kutoka Taasisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Tume ya Nguvu za Atomiki wakifuatilia majadiliano na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani), kikao kazi hicho kimefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma.


Hivyo makala Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini

yaani makala yote Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/waziri-mpina-akutana-na-taasisi-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini"

Post a Comment

Loading...